Halmashauri ya Mji Njombe ina jumla ya Ng’ombe wa Asili 29,171 , Ng’ombe wa Maziwa 6,560, Mbuzi 18,164, Mbuzi wa Maziwa 384, Kondoo 3,740, Nguruwe 6,194, Mbwa 5,225, Punda 7,630, Paka 7,110, Simbilisi 29,205, Sungura 8, Kuku wa asili 18,510, Kuku wa Kisasa 35,789, Njiwa 679 na Farasi 9. Pia eneo linalofaa ni hekta 34,570, pandwa ni hekta 157.
Kwa upande wa ufugaji wa samaki, Halmashauri ya Mji Njombe ina jumla ya wafugaji 96 wa samaki ambapo kwa ujumla wao wana mabwawa 156 ya samaki aina ya perege.
Kwa upande wa miundo mbinu ya Mifugo, Halmashauri ya Mji Njombe ina Maabara ya Mifugo 1 inayofanya kazi, Machinjio Kubwa ya Ng’ombe na Mbuzi 1, majosho 12 yaliyotawanyika katika Karibu kata zote ambayo 8 yanamilikiwa na Serikali na majosho 4 ya Watu Binafsi.
Pia katika Halmashauri ya Mji Njombe Kuna Kiwanda Kikubwa cha Maziwa chenye uwezo wa kusindika lita 6000 kwa siku ambapo mazao mbalimbali ya maziwa yanazalishwa kama Mtindi (Yogurt), Maziwa fresh (Pasteurized milk), Jibini( Cheese) za aina mbalimbali kama Kachota, Asiago na Provoloni. Kiwanda hicho kina Maabara ya kisasa yenye uwezo wa kupima ubora wa maziwa.
UPEKEE WA HALMASHAURI YA MJI NJOMBE KATIKA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI:
Katika sekta ya Mifugo na Uvuvi, Ufugaji wa ng’ombe wa Maziwa na Kuku ndizo shughuli ya pekee ambapo kuna wafugaji wenye uelewa mkubwa na pia kuna ng’ombe wa maziwa aina ya Ayrshire, Friesian na Chotara ambapo wanauwezo wa kutoa lita 5 hadi 20 kwa siku. Mfugaji wa Kuku ana Shamba la kuku lenye kuku wa asili 600 na Kisasa 1200
SHUGHULI KUU ZA IDARA YA MIFUGO NA UVUVI
WAFANYAKAZI WA IDARA YA MIFUGO NA UVUVI
Idara ya Mifugo na Uvuvi ina jumla ya wafanyakazi 26 ambapo watumishi 10 wapo Ofisi kuu na Watumishi 16 wapo katika ngazi ya Kata na Mitaa/Vijiji.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe