Naibu Waziri OR-TAMISEMI Dkt, Festo Dugange amefurahishwa na utekelezaji wa miradi ya afya ikiwa ni ujenzi wa vituo 02 vya afya kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri na utoaji wa mikopo asilimia 10 kwa vikundi vya Wanawake, vijana na walemavu.
Katika ziara yake kwenye Halmashauri ya Mji Njombe ambapo alizungumza na watumishi wa afya Kibena Hospitali na kukagua utoaji wa huduma katika Hospitali hiyo, Dkt. Dugange amesema kuwa Halmashauri ya Mji Njombe imepiga hatua kubwa hususani katika sekta ya afya kwa kuweza kujenga vituo vya afya viwili kwa kutumia mapato ya ndani ya Halmashauri, kuboresha miundombinu katika zahanati,ujenzi wa zahanati na ufungaji wa mifumo ya kukusanyia mapato katika vituo vya afya Jambo linaloongeza mapato ya Kituo na kuendelea kusogeza huduma karibu na Wananchi."Halmashauri ziige mfano kutoka Halmashauri ya Mji Njombe. Nikupongeze Mkurugenzi kwa Kasi hii.Kupitia Miradi hii jamii itakwenda kunufaika niwapongeze "Alisema Naibu Waziri
Wakati akikagua Vikundi vya Wanufaika wa Mikopo ya Wanawake Vijana na Walemavu ambapo alitembelea kikundi Cha Wanawake na Kikundi Cha Vijana NJAVIDA Dkt, Dugange amesema Serikali imetoa mikopo hiyo ili kuhakikisha kuwa Wananchi Wanajipatia kipato."Serikali haiwezi kuajiri vijana wote lazima wengine tujiajiari.Niwapongeze Halmashauri mmeweza kutoa mikopo.Kikundi Cha Vijana NJAVIDA Halmashauri imewapatia milioni 30 na wamenunua mashine za useremala kwa ajili ya kutengeneza samani.Hii ikawe chachu kwa Vijana ambao wanasubiri kuajiriwa"Alisema Naibu Waziri
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe