Elimu ya manufaa yatokanayo na mpango wa Urasimishaji inayoendeshwa na MKURABITA Kwenye Halmashauri zinazonufaika na mpango huo bado ni changamoto kubwa inaowakabili Wananchi kwani wengi wao bado hawana uelewa wa kutosha juu manufaa ya Urasimishaji.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Dkt.Mary Mwanjelwa (Mb) kwa Watendaji wa Halmashauri kwenye ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Mji Njombe iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya MKURABITA katika Halmashauri hiyo na kuwataka Watendaji kwenye Halmashauri zinazonufaika kutoa elimu kwa umma juu ya manufaa ya Urasimishaji Ardhi na Biashara zao.
Dkt. Mwanjelwa amesema kuwa licha ya kuwa Halmashauri imefanya vizuri katika kutekeleza mpango huo bado elimu iliyotolewa haijitoshelezi jambo ambalo lisipotiliwa mkazo linaweza kusababisha migogoro.
“MKURABITA ni ya Wananchi, Urasimishaji ni kwa ajili ya Wananchi. Waelezeni bayana Wajibikeni kwa Wananchi kwa kutoa huduma ipasavyo.”Alisema Mary Mwanjelwa.
Aidha, Dkt. Mwanjelwa ametoa maelekezo kwa Wasimamizi wa Urasimishaji kuhakikisha kuwa mashamba ya miti na parachichi yanapimwa kwa kadri wananchi walivyoomba ili Wananchi waweze kupata hati za mashamba yao.
Wakielezea kwa Nyakati tofauti tofauti baadhi ya Wanufaika wa Mpango wa Urasimishaji “Chambinga Workshop, Nahala na Mama Seki” wamesema kuwa manufaa waliyoyapata ni pamoja na kupata mikopo katika Taasisi mbalimbali za kifedha jambo ambalo limewasaidia kuendeleza biashara zao na kuboresha hali za maisha katika familia zao.
Halmashauri ya Mji Njombe imefanikiwa Kurasimisha viwanja na nyumba 8,782 na jumla ya wafanyabiashara 129 waliweza kupatiwa mikopo yenye thamani ya shilingi 899,499,488/= kutoka Taasisi mbalimbali za kifedha yote ikiwa ni manufaa yaliyotokana na zoezi la Urasimishaji.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe