Halmashauri ya Mji Njombe imekabidhi meza na viti 280 vyenye thamani ya Shilingi milioni ishirini na tatu laki mbili na elfu arobaini kwa ajili ya Shule 4 za Sekondari zilizopo katika Halmashauri hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wakati wa makabidhiano hayo Afisa Elimu Sekondari Rehema Nswila amesema kuwa Halmashauri kupitia mapato ya ndani ilitenga kiasi cha Shilingi milioni 30 kwa ajili ya ununuzi wa meza, viti, vitanda kwa ajili ya kutatua changamoto katika Shule za Sekondari zilizokuwa na uhitaji.
“Wote tunatambua jitihada kubwa alizozifanya Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika sekta ya elimu.Elimu bila malipo imepelekea kuwepo na ongezeko kubwa la Wanafunzi katika Shule zetu. Na sisi kama Halmashauri tupo kwenye mapambano ya kuhakikisha kuwa kila Mwanafunzi anapata Elimu bora ikiwa ni sambamba na kupata mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia.Kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri tunakabidhi meza na viti 280. Tuhakikishe kuwa Wanafunzi hawafanyi uharibifu na zinatumika vyema.” Alisema
Editha John Mkuu wa Shule ya Sekondari Yakobi, Alex Chengula Shule ya Sekondari Uwemba, James Tamaa Mbele na Alex Tchwodzie kutoka Shule ya Sekondari Luhololo wameishukuru Halmashauri kwa kuwapatia samani hizo ambazo zitasaidia kutatua changamoto iliyokuwepo kwa kiasi kikubwa.
“Shule ya Sekondari Luhololo kwa sasa tunakamilisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na sasa tumepata madawati na meza themanini, yatakayoenda kuwekwa kwenye madarasa hayo. Badala ya Wananchi kuchangia meza na madawati tutaendelea na miradi mingine kwani Halmashauri imeshatusogeza. Alisema Mwalimu Alex
Halmashauri ya Mji Njombe kupitia mapato ya ndani imekabidhi madawati na meza 80 kwa Shule ya Sekondari Uwemba, Yakobi na Luhololo na madawati na meza 40 kwa ajili ya Shule ya Sekondari Mgola na hivyo kufanya idadi yake kuwa 280.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe