• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Mipango
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

Halmashauri ya Mji Njombe Yatoa Milioni Mia Saba kwa Vikundi 72

Tarehe iliyowekwa: December 2nd, 2020

Halmashauri ya Mji Njombe imetoa kiasi cha Shilingi milioni mia saba laki tisa kwa vikundi 72 vya kiuchumi vya Wanawake, Vijana na Walemavu kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2020/2021.

Kiasi hicho cha fedha kinatokana na makusanyo ya mapato ya ndani ambapo kiasi cha Shilingi milioni 120 zimechangiwa, huku kiasi kilichosalia ikiwi ni fedha za marejesho.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mfano wa hundi kwa vikundi hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhandisi Marwa Rubirya amevitaka vikundi hivyo kufanya matumizi sahihi ya mikopo hiyo ili kuwa endelevu na  kufanya marejesho kwa wakati jambo litakaloviwezesha vikundi vingine kukopa.

“Mikopo hii ikatumike kwa malengo yaliyokusudiwa. Sio mnatumia fedha hizi kama kikundi mkifika kule mnagawana.Mwingine anaenda kununua baiskeli mwingine anaenda kulipa ada ya shule.Hayo sio malengo ya mkopo huu.”

Awali akiwasilisha taarifa ya hali ya utoaji wa mikopo katika Halmashauri Afisa Maendeleo ya Jamii Enembora Lema amesema kuwa Hali ya utoaji wa mikopo katika Halmashauri imeendelea kuimarika kila wakati kwani kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Halmashauri ilitoa TSH. 375,733,00, Mwaka 2019/2020 ilitoa TSH. 676,300,000 na Mwaka 2020/2021 kwa robo ya kwanza pekee Halmashauri imeanza kwa kutoa TSH  700,900,000/=

Kwa upande wao mwakilishi kutoka kundi la walemavu na wanawake wamesema kuwa ni vyema wanavikundi kutumia fedha hizo kuchochea shughuli za maendeleo jambo litakalopelekea kufanya marejesho kwa wakati.

“Tukisema tuchepushe kidogo hii fedha marejesho yatatushinda.Tutaanza kulalamika fedha ya Halmashauri inamkosi kumbe mkosi ni sisi wenyewe.”Alisema Mwakilishi wa Wanawake.

Aggrey Chatanda ni Mwakilishi kutoka Kundi la vijana amesema kuwa fedha hizo zitakwenda kuongezea nguvu kwenye mradi wa nyuki ambao tayari umeanza.

Utaratibu wa Utoaji wa mikopo bila riba kwa vikundi vya Wanawake,Vijana na Wenye ulemavu ulianzishwa ili wanufaika waweze kupata mitaji na kufanya uwekezaji katika shughuli za kiuchumi, Mathalani katika Kilimo,Ufugaji,Uvuvi na kuanzisha viwanda vidogo vidogo na hatimaye kuweza kuboresha Maisha kuanzia ngazi ya Familia,Jamii na Taifa.

Matangazo

  • MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021,SHULE ZA KITAIFA, TEULE NA KUTWA WANAFUNZI WA HALMASHAURI YA MJI NJOMBE December 18, 2020
  • FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021, SHULE ZA SEKONDARI KATIKA HALMASHAURI YA MJI NJOMBE December 15, 2020
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA September 21, 2020
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Mvua yaleta maafa kwa familia 6 katika Kijiji cha Ikisa

    January 16, 2021
  • Halmashauri ya Mji Njombe Yashika Nafasi ya Nne Matokeo Kidato cha Nne

    January 15, 2021
  • Halmashauri ya Mji Njombe yatoa taulo za kike kwa Shule za Sekondari

    January 07, 2021
  • Jafo afurahishwa ujenzi wa Vituo vya Afya Njombe Mji

    December 22, 2020
  • Angalia zote

Video

Makala ya utekelezaji miradi ya maendeleo 2020 Halmashauri ya Mji Njombe
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe