Jumla ya Miradi tisa yenye thamani ya zaidi shilingi bilioni sita imekaguliwa, kuwekewa mawe ya msingi na kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru Septemba 18, 2019 katika Halmashauri ya Mji Njombe na kubainika kutokuwa na dosari katika utekelezaji wa miradi hiyo.
Akizungumza mara baada ya kufanya ukaguzi wa shughuli za ujenzi unaoendelea wa soko la kisasa Njombe, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mzee Mkongea Ally ameipongeza Halmashauri ya Mji Njombe kwa kusimamia kwa uadilifu miradi hiyo na kuitaka Halmashauri kuendelea na usimamizi huo madhubuti katika utekelezaji wa miradi mingine ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri .
“Tungesema tuitishe harambee kiasi hiki cha bilioni tisa kisingeweza kukamilika kwa wakati. Mheshimiwa Rais amehakikisha anaweza kuleta fedha hizi za ujenzi wa soko ili Wananchi waweze kunufaika. Tuendelee kumuunga mkono Mheshimiwa Rais kwa kazi anazofanya.Niwapongeze pia Wataalamu kwa kazi ya uaminifu, kazi iliyotukuka ni jambo jema sana. Niwaombe mkamilishe ujenzi wa soko hili kwa wakati lakini wale watakaopewa vizimba katika soko hili basi wafikiriwe wale watu ambao hali zao ni wanyonge. Wasitokee vigogo wakachukua vizimba halafu wao wanapangisha kwa watu wengine.”Alisema Mzee Mkongea Ally.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini Edward Franz Mwalongo Alisema kuwa Ujenzi Wa Soko Hilo Umeanza Mwaka 2018 Kwa ajili Ya Kutoa Huduma Kwa Wananchi Wa Mkoa Wa Njombe Unaotarajia Kukamilishwa Mwezi Ujao Na Kumuomba Kiongozi Wa Mbio Za Mwenge Kupeleka Shukurani Kwa Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
“Ndani ya mwaka mmoja wa uongozi wa Mheshimiwa Rais Magufuli tumeweza kupata soko la kisasa Njombe, Mwenyewe umeona picha za awali kabla ya ujenzi wa soko hili.Soko hili likikamilika litakuwa ndio jengo litakalobeba sura ya mji wa njombe linataraji kuwa na Wafanyabiashara zaidi ya 700 jambo ambalo litakuza uchumi wa Wakazi wa Njombe na kitakuwa chanzo kikubwa cha mapato cha Halmashauri.
Naye Mkuu Wa Wilaya Ya Njombe Bi. Ruth Msafiri Akizungumza Kabla Ya Kwenda Kukabidhi Mwenge Wa Uhuru Katika Wilaya Ya Makete Ametaja Takwimu Ya Maambukizi Ya Virusi Vya UKIMWI Kupungua Kwa Wanaume Kwani Kati Ya Watu 147 Waliopima Kwenye Mkesha Wa Mwenge Wanawake wakiwa 46 na Wanaume 101, Ni Watu 5 Wanawake Wawili Na Wanaume Watatu walibainika kuwa na maambukizi mapya ya UKIMWI.
“Kwa mara ya kwanza wanaume wamejitokeza kwa wingi kupima. Hii inaonesha ni kwa jinsi gani Kampeni ya Pimba, Jitambue Ishi ilivyokuwa na manufaa” Ruth Msafiri alisema
Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Inaendelea Na Jitihada Za Kutekeleza Malengo Matano Ya Darubini Ya Dira Ya Taifa Ya Maendeleo Mwaka 2025 Ikiwemo Lengo Namba Moja La Dira Ya Taifa La Kuboresha Hali Ya Maisha Ya Watanzania.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe