• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Halmashauri ya Mji Njombe
Halmashauri ya Mji Njombe

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI Halmashauri ya Mji Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu na uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mazingira na Usafishaji
      • Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu.
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Election
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Utamaduni,Sanaa na Michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

Wafugaji wa Samaki Njombe wapatiwa mafunzo juu ya ulishaji

Tarehe iliyowekwa: February 12th, 2020

Akielezea madhumuni ya mafunzo ya ulishaji samaki kwa wafugaji, Daktari Gloria Yona ambaye ni Mtafiti Mwandamizi wa maswala ya Samaki amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga katika kumsaidia Mfugaji wa hali ya chini kuweza kumudu gharama za chakula kwa kutumia malighafi zinazomzunguka na kuepuka matumizi ya vyakula vya madukani ambavyo vimekuwa ni vya gharama kubwa.

Baadhi ya wafugaji samaki waliopata mafunzo hayo akiwemo Emmanuel Kinyamagoha, Theodori Mlowe wamesema kuwa mafunzo hayo yamekuwa ni ya manufaa kwao kwani zoezi la ulishaji samaki lilikuwa ni changamoto kubwa iliyokuwa inawakabili jambo lililokuwa likipeleka kutumia fedha nyingi kununua vyakula vya samaki kwenye maduka na bila kuzingatia utaalamu wa uchanganyaji chakula wakati wa ulishaji.

“Shida kubwa ilikuwa ni upatikanaji wa elimu. Watu wengi katika Mkoa wetu wanahamasika kufanya shughuli za ufugaji samaki. Tuchangamkie fursa hii kwani pia si kutuongezea kipato tuu bali kusaidia kupunguza tatizo la udumavu unaoukabili Mkoa wetu wa Njombe.”Alisema Lupenza mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo.

Awali akifungua mafunzo hayo Katibu Tawala Wilaya ya Njombe George Emmanuel amesema kuwa ni vyema kuitumia fursa hiyo ya mafunzo ipasavyo kwani itasaidia katika kuleta maendeleo ya mtu mmoja mmoja na hivyo kuendeleza mnyororo wa thamani.

“Niwaombe Watendaji kuhakikisha kuwa baada ya mafunzo haya ufuatiliaji unafanyika kwa wafugaji wa samaki ili kuweza kutatua changamoto zitakazokuwa zinawakabili” Alisema Katibu Tawala.

Licha ya kuwepo kwa hamasa kubwa ya ufugaji samaki katika Halmashauri ya Mji Njombe, changamoto kubwa imekuwa ni wafugaji wengi kutowahusisha wataalamu wa mifugo ili kuweza kupata ushauri wa Kitaalamu jambo ambalo limepeleka wafugaji wengi kufanya ufugaji wa mazoea na hata wakati mwingine kuingia gharama nyingi katika kununua vifaranga vya samaki.






Matangazo

  • KUITWA KAZINI NA MAFUNZO TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI JIMBO LA NJOMBE MJINI. October 21, 2025
  • TANGAZO LA UCHAGUZI JIMBO LA NJOMBE MJINI. October 19, 2025
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. April 18, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • RC MTAKA AONGOZA MAOMBI YA AMANI KWA TAIFA.

    November 07, 2025
  • MSIMAMIZI WA UCHAGUZI JIMBO NJOMBE MJINI AFUNGUA MAFUNZO KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA .

    October 26, 2025
  • MAKARANI WAONGOZAJI WAPIGA KURA 366 WAAPISHWA NA KUPATIWA MAFUNZO JIMBO LA NJOMBE MJINI.

    October 25, 2025
  • KUBWA KULIKO KUWAHI KUTOKEA NJOMBE MJINI

    October 20, 2025
  • Angalia zote

Video

TANGAZO LA UCHAGUZI JIMBO LA NJOMBE MJINI.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe