1.0 Utangulizi
Halmashauri ya Mji Njombe ni moja kati ya Halmashauri tatu (3) zinazounda Wilaya ya Njombe, Halmashauri nyingine ni Mji Makambako na Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Halmashauri hii ilianzishwa mwaka 2007 baada ya Halmashauri ya Wilaya ya Njombe kugawanywa. Kwa upande wa Mashariki imepakana na Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Kaskazini imepakana na Halmashauri Wilaya ya Wanging`ombe, Magharibi imepakana na Wilaya ya Makete na Wanging`ombe, Kusini imepakana na Wilaya ya Ludewa na Mkoa wa Ruvuma. Halmashauri ya Mji Njombe ina ukubwa wa mita mraba 3,212 za eneo linalojumuisha Tarafa 2, Kata 13;Kata (3) ni za mjini na (10) ni za Vijijini, Vijiji 44 na Mitaa 28.
1.1 Idadi ya Watu
Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Halmashauri ya Mji Njombe ilikuwa na watu wapatao 130,223 (Me 61,112 na Ke 69,111). Kwa mwaka 2016 idadi ya watu inakadiriwa kuwa 134, 801 (Wanawake 71,541 na Wanaume 63,260). Hii ni kutokana na ongezeko la ukuaji wa idadi ya watu la asilimia 0.8 kwa mwaka.
1.2 Hali ya hewa
Kwa jumla hali ya hewa ya Halmashauri ya Mji wa Njombe ni nzuri kwa maisha na uzalishaji. Kipindi cha mvua huanza Mwezi Oktoba hadi Aprili ambapo mvua hufikia kati ya milimita 1200 hadi 1400 kwa Mwaka. Aidha, baadhi ya maeneo hupata mvua za vuli katika kipindi cha mwezi Septemba. Aidha kuna kipindi cha baridi ambapo joto hushuka hadi (40C) kipindi hiki huanza mwezi Mei hadi Agosti; na kipindi cha majira ya joto (280C) huanza mwezi Novemba hadi Machi.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe