• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu na uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mazingira na Usafishaji
      • Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu.
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Election
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Utamaduni,Sanaa na Michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

Maliasili

Halmashauri ya Mji wa Njombe ina misitu ya asili 15 inayokadiriwa kuwa na ukubwa wa hekta 3,014 na pia kuna mito mikubwa na midogo isiyokauka kwa kipindi chote cha mwaka. Misitu hii ina aina mbalimbali za miti zinazotoa maua yanayowezesha upatikanaji wa asali yenye ubora wa kipekee. Hata hivyo yapo mazao mbalimbali ya chakula na biashara kama mahindi, alizeti, viazi vitamu na miti mingi ya matunda ambayo hutoa maua yanayosaidia katika upatikanaji wa poleni.

Hata hivyo katika kuhakikisha kuwa rasilimali ya nyuki inaendelezwa ili ichangie katika kuinua kipato cha jamii na kushiriki katika utunzaji wa mazingira endelevu, huduma mbalimbali zinatolewa kwa wananchi. Huduma hizo ni pamoja na :- Utoaji wa hamasa na elimu ya ufugaji wa nyuki, Kutoa vifaa vitumikavyo katika ufugaji wa nyuki, ikiwemo mizinga ya kisasa na mavazi ya kurinia kwa vikundi vya wafugaji wa nyuki, Kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vikundi vya wafuga nyuki.

Hadi mwezi February/2015, Halmashauri ya Mji wa Njombe ina mizinga ya kisasa ya ufugaji nyuki ipatayo 1,363 ya kisasa na 4,648 ya kienyeji na wafugaji wa nyuki wapatao 357 na idadi hii inazidi kuongezeka kutokana na hamasa inayoendelea kutolewa.

UFUGAJI WA NYUKI

Ufugaji wa nyuki ni taaluma inayotumia rasilimali ya nyuki (wanaouma na wasiouma) na mimea katika kuzalisha asali, nta, gundi ya nyuki, maziwa ya nyuki, majana, sumu ya nyuki, chavua na nyuki wenyewe.

FAIDA ZA UFUGAJI NYUKI

Mdau wa ufugaji wa nyuki anaweza kufaidika na taaluma hii kama vile:-

  • Kuongeza pato lake na jamii yake.
  • Kuhifadhi mazingira yanayozunguka eneo analoishi.
  • Kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula kwani nyuki huchavusha mimea wakati akitafuta chavua.
  • Huongeza ubora wa matunda na mbegu za mimea kutokana na uchavushaji.
  • Hutunza ikolojia na kuhifadhi bioanuai za wanyama na mimea katika eneo husika .
  • Shughuli ya ufugaji wa nyuki huweza kufanywa na mtu mwenye hali, umri na jinsia yoyote (mlemavu, mzee au kijana).
  • Mazao ya nyuki yaweza kuwa malighafi kwa viwanda vingine vidogovidogo kama vile nta hutumika katika viwanda vya kutengeneza mishumaa, sabuni na vipodozi.
  • Upatikanaji wa ajira kwa vijana, wanawake na wazee.

 

FURSA ZA UFUGAJI NYUKI ZILIZOPO

  • Uwepo wa misitu ya hifadhi inayofaa kwa ufugaji wa nyuki.
  • Upatikanaji wa vyanzo mbalimbali vya maji kama vile mabwawa na mito mikubwa na midogo inayotiririsha maji katika kipindi kirefu cha mwaka.
  • Uwepo wa nguvukazi ya kutosha na utayari wa wananchi kufuga nyuki.
  • Uwepo wa Sera ya Taifa ya ufugaji nyuki ya mwaka 2002, sheria ya ufugaji nyuki na kanuni zake.
  • Upatikanaji rahisi wa makundi ya nyuki, hususani wanaouma, katika maeneo mbalimbali ya mji wetu.
  • Uwepo wa kilimo cha mazao ya chakula na biashara, kilimo cha miti ya matunda ambayo huwezesha upatikanaji wa asali iliyo nzuri.

CHANGAMOTO ZINAZOKABILI KITENGO CHA NYUKI

  • Uvamizi na uchomaji ovyo wa misitu kutokana na shughuli za kilimo.
  • Kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu ufugaji wa kisasa wa nyuki.
  • Ukosekanaji wa mitaji kwa wafugaji kwa ajili ya kuendesha shughuli hii.
  • Uzalishaji mdogo wa asali kukidhi soko la ndani na la nje ya nchi.
  • Uhaba wa upatikanaji wa vifaa maalum kwa ajili ya shughuli za ufugaji nyuki, mfano vifaa na mavazi ya kinga.
  • Uhaba wa wataalam katika sekta hii.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI,UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI. April 25, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UBORESHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA. December 20, 2024
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. April 18, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKUU WA WILAYA NJOMBE MHE. JUMA SWEDA ATOA WITO KUHUSU CHANJO YA PILI YA POLIO.

    April 29, 2025
  • AFISA MWANDIKISHAJI JIMBO LA NJOMBE MJINI AKUTANA NA VYAMA VYA SIASA

    April 24, 2025
  • ZIARA YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YA NJOMBE KUKAGUA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2025

    April 04, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Njombe awaonya wenyeviti kuhusu uharibifu wa miradi ya maendeleo

    February 15, 2025
  • Angalia zote

Video

WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA KUJITUMA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe