Akizungumza wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Serikali kwa vyombo vya habari Mkoani Njombe, Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema kuwa Mkoa wa Njombe kwa kipindi cha miezi 9 cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan umepokea shilingi Bilioni 375.4 fedha ambazo zimeekelezwa katika kutekeleza miradi kwenye sekta ya Barabara, Maji, Elimu na Afya
“Njombe ni Mkoa wa Kilimo kwa Sehemu kubwa, ni moja ya Mikoa inayotegemewa kuzalisha chakula na kwa sasa ni Mkoa ambao unaibuka kwa kasi kubwa kuzalisha mazao ya biashara vikiwemo viazi, mbao, na parachichi. Sehemu kubwa ya fedha zilizotolewa hapa Njombe zimeelekezwa katika ujenzi wa barabara ili kurahisisha shughuli za maendeleo kwa Wananchi” Alisema Msigwa.
Katika sekta ya kilimo cha miti na parachichi Msemaji wa Serikali amesema kuwa takwimu za mwaka jana 2021 Mkoa wa Njombe umeweza kukusanya mapato ya shilingi Bilioni 7 na milioni 423 kutokana na uvunaji wa mbao na kwa upande wa kilimo cha parachichi tani 9,402 zimevunwa na kuuzwa na hivyo kupelekea shilingi Bilioni 15.6 kulipwa kwa Wakulima wa Parachichi.
Akitoa taarifa ya miradi iliyotekelezwa kupitia fedha za mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano ya UVIKO-19 Msigwa amesema kuwa Mkoa wa Njombe ulipokea kiasi cha shilingi Bilioni 7 na milioni 160, ikiwa ni kufanikisha ujenzi wa miundombinu ya Afya, E limu ambapo mpaka sasa jumla ya vyumba vya madarasa 192 vimejengwa katika Shule za Sekondari za Mkoa wa Njombe, Shule Shikizi 32 na Mabweni 03 kwa watoto wenye mahitaji maalumu.
Akitoa taarifa ya mradi wa makaa ya Mawe na Chuma wa Liganga na Mchuchuma ulipo Wilaya ya Ludewa Msigwa amewahakikishia Wananchi wa Njombe kuwa Serikali ya awamu ya sita inaendelea na majadiliano kati ya Mwekezaji na Serikali ili kuhakikisha kuwa maslahi ya Wananchi wa Njombe na Taifa yanalindwa kabla ya utekelezaji wa mradi na Serikali imeendelea kusukuma kukamilika kwa majadiliano hayo ili mradi uweze kutekelezwa kwa haraka.
Kwa upande wa Sekta ya maji Msemaji wa Serikali amesema kuwa mpaka sasa hali ya usambazaji wa maji ni wastani upo wastani wa asilimia 72.3 Vijijini na silimia 86 Mijini licha ya kuwepo na changamoto katika kipindi cha mwisho wa mwaka 2021 kutokana na upungufu wa mvua ambapo kwa sasa hali ya huduma ya maji imeanza kutengemaa baada ya kuanza kwa mvua. Hata hivyo Serikali imeendelea na dhamira yake ya kuchukua maji kutoka kwenye vyanzo vikubwa vya maji na mito ili kuhakikisha kuwa Wananchi wanapata maji ya uhakika.
Katika mkutano huo na vyombo vya habari Waandishi wa Habari na Wananchi waliokuwa wakifuatilia matangazo hayo mubashara pia walipata nafasi ya kuuliza maswali na kupatiwa ufafanuzi wa hoja mbalimbali.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe