• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Mipango
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

DC NJOMBE AONGOZA ZOEZI LA UPANDAJI MITI NA KUPIGA MARUFUKU UENDELEZAJI VYANZO VYA MAJI

Tarehe iliyowekwa: June 5th, 2022

Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mheshimiwa Kissa Gwakisa Kasongwa leo ameongoza Wananchi na Watumishi wa Mkoa wa Njombe katika zoezi la upandaji miti aina ya mivengi kwenye eneo oevu la Nyikamtwe  Mtaa wa Lunywanywi  wakati wa maadhimisho ya siku ya mazingira dunia ambapo huadhimishwa kila tarehe  5 mwezi Juni.

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo yenye kauli mbiu “TANZANIA NI MOJA TU, TUNZA MAZINGIRA"  Mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Gwakisa  akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Njombe amesema kuwa Mkoa wa Njombe ni miongoni mwa Mikoa iliyobarikiwa kuwa na vyanzo vingi vya maji ambavyo idadi yake inakadiriwa kuwa 4436 ambapo vyanzo hivyo vinahitaji kuendelezwa na kutunzwa kwa kupanda miti rafiki na maji ili kuendeleza uhifadhi wa mazingira katika maeneo hayo.

Kissa amesema kuwa, Uwepo wa vyanzo hivi vya maji unamanufaa makubwa sio kwa Mkoa wa Njombe Pekee tu bali hata kwa Nchi nzima kwani vyanzo hivi vitakwenda kupunguza changamoto kubwa ya maji na pia kuendeleza uhifadhi wa mazingira katika maeneo yetu. Tukumbuke kuwa Mkoa wa Njombe ni miongoni Mikoa yenye vyanzo vikubwa nchi vya maji na ambavyo vinatarajiwa kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kufanikisha uwepo wa maji katika bwawa la Mwalimu Nyerere ambalo litakwenda kutumika katika uzalishaji wa umeme kwa ajili ya manufaa yetu.

Katika hatua nyingine Mheshimiwa Kissa amepiga marufuku Wananchi kuendeleza shughuli zozote za kibinadamu katika  maeneo ya vyanzo vya maji ili kuendeleza kutunza rasilimali hizo muhimu.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Bi. Judica Omary amesema kuwa zoezi la upandaji wa miti hiyo rafiki wa mazingira  unafanyika ili kuongeza uimarishaji wa uhifadhi wa mazingira katika bonde la Nyikamtwe.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti, Diwani wa Kata ya Mjimwema Nestory Mahenge na Mwenyekiti wa  Mtaa huo wa Lunyanywi Laurent Lupenza wamesema kuwa ni faraja kubwa kwa tukio hilo la upandaji miti kufanyika katika eneo hilo kwani itasaidi eneo hilo kuendelea kuwa katika hali yake ya asili lakini pia wameahidi kuendelea kutoa elimu kwa jamii inayozunguka eneo hilo na Wananchi wa Mtaa huo kutunza na kuhifadhi eneo hilo muhimu.

Maadhimisho ya siku ya mazingira duniania huadhimishwa kwa Viongozi na Wananchi kushiriki katika shughuli mbalimbali za uhifadhi wa mazingira lengo ikiwa ni kuvilinda vyanzo mbalimbali vya maji na kuvinusuru juu ya uharibifu unaofanywa na shughuli mbalimbali za Kibinadamu.

 

Matangazo

  • TANGAZO LA AJIRA ZA MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 06, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI KWENYE ZOEZI LA ANWANI ZA MAKAZI HALMASHAURI YA MJI NJOMBE March 25, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI May 25, 2022
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DC AFURAHISHWA NA MWENENDO WA UTEKELEZAJI WA MIRADI KATA YA MATOLA

    June 10, 2022
  • ZIARA YA DC KISSA YAWAIBUA WANANCHI KUPATA CHANJO YA UVIKO

    June 09, 2022
  • DC NJOMBE AIELEKEZA IDARA YA ARDHI KUSHUGHULIKIA MGOGORO WA ARDHI NDANI YA WIKI MBILI

    June 08, 2022
  • DC NJOMBE AONGOZA ZOEZI LA UPANDAJI MITI NA KUPIGA MARUFUKU UENDELEZAJI VYANZO VYA MAJI

    June 05, 2022
  • Angalia zote

Video

Makala ya utekelezaji miradi ya maendeleo 2020 Halmashauri ya Mji Njombe
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe