Serikali nchini Tanzania imejipanga kutengenezea mazigira rafiki kwa watu wenye ulemavu kwa kuwajengea uwezo wa kiuchumi pamoja kuwatengenezea miundombinu rafiki na wezeshi ya kujipatia kipato.
Hayo yamezungumzwa Novemba 23,2023 na Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Bi.Judica Omari katika ufunguzi wa Kongamano la Ugemaji kwa Watu Wasioona kuelekea kilele cha Siku ya Fimbo Nyeupe yanayofanyika kitaifa Mkoani Njombe ambapo Bi .Judica kwa niaba ya Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe amesema Serikali imejipanga kuhakikisha walemavu wote nchini wanapata fursa mbalimbali za uchumi Pamoja na kuwatengenezea mazingira rafiki na miundombinu iliyo bora ya ufanyaji wa kazi za kujiingizia kipato.
Akiendelea kuzungumza Bi Judica ameweka wazi mikakati ambayo serikali imefanya ya kuhakikisha walemavu wanapata mikopo ya Halmashauri ambayo haina riba yeyote kupitia mapato ya ndani ambapo kwa mwaka wa fedha 2020/2021 hadi 2022/2023 serikali mkoani Njombe imetoa kiasi cha fedha shilingi milioni 840,899,416/= kutoka mapato ya ndani ya halmashauri ,kwa ajili ya kuwa wezesha watu wenye ulemavu katika shughuli mbalimbali za uchumi.
Aidha Katibu Tawala Mkoa wa Njombe ameziomba Halmashauri zote Nchini kuhakikisha zinatenga maeneo kwa ajili ya shughuliza za uchumi za vikundi mbalimbali vya watu wenye ulemavu Pamoja na kushirikiana na viongozi wa chama cha walemavu (TLP Tanzania League of Blind-Chama cha wasioona Tanzania).
Kwa upande wake Rased Mftaa Mkurugenzi wa kitengo cha Huduma kwa watu wenye ulemavu amesema kuwa shughuli mbalimbali ambazo zimefanyika katika kongamano hilo ni pamoja na taratibu za mikopo ya elimu ya juu, bima ya afya Pamoja na fursa za kiuchumi kwa wasioona .
Maadhimisho hayo kwa mwaka 2023 yanayofanyika kwa siku tatu ambapo kilele chake ni Novemba 24,2023 Kauli Mbiu ya maadhimisho hayo inasema, “UPATIKANAJI WA TEKNOLOJIA FIKIVU KATIKA UJENZI WA UCHUMI WA KIDIJITALI, NI MKOMBOZI WA MTU ASIONA NA TAIFA “
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe