Katibu tawala Mkoa wa Njombe Ndugu Judica Omary Novemba 10,2023 ametembelea hospitali ya Halmashauri ya Mji Njombe Kibena na kukagua ujenzi wa wodi ya huduma kwa akina mama ,watoto wachanga na watoto njiti.
Katibu tawala ameipongeza serikali ya mtaa uongozi wa hospitali na Halmashauri ya mji Njombe kwa kusimamia ujenzi wa jengo hilo ambalo limekamilika kwa asilimia 99.9.
Jengo hilo litakuwa na uwezo wakupokea na kuhudumia watoto njiti 25 kwa wakati mmoja.
“Wakati tumekuja hapa tuliona jengo wanalohudumiwa watoto njiti na ule ufinyu uliopo lakini sasa tunaona hospitali ya Mji inaenda kuwa bora zaidi hata wazazi watakao kuja hapa watafurahi,hapa kweli mmefanya kazi nzuri.”Alisema Bi.Judica Omary
Aidha amemuelekeza mhandisi wa ujenzi Halmashuri ya Mji Njombe kushirikiana na uongozi wa hospitali na kijiji ili kufanya ukaguzi wa mwisho, kuweza kubaini maeneo ambayo yanahitaji kuwekwa sawa ili jengo hilo lizinduliwe kwa ajili yakuanza kutoa huduma.
“Mhandisi nakuomba hatua za mwisho hizi fundi amemaliza ,lakini snacks zipo vitasa ,socket na maeneo mengine pitia uone,na kama fundi alifanya vibaya aitwe arekebishe,tuweke utayari wa asilimia mia moja.”
Halmashauri ya Mji Njombe kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 ilipokea fedha shilingi 150,000,000/= kupitia serikali ya kijiji, kwa ajili ya ujenzi wa wodi yakuhudumia akina mama ,watoto wachanga na watoto njiti katika Hospitali ya Mji Kibena kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe