Kila Disemba Mosi ya Kila Mwaka Dunia huadhimisha siku ya UKIMWI Duniani ambapo leo Katika Halmashauri ya Mji Njombe Maadhimisho hayo yenye Kauli Mbiu “Imarisha Usawa” ambapo Takwimu zinaonyesha kuwa Mkakati wa kuzuia Virusi vya UKIMWI toka kwa Mama kwenda kwa Mtoto umeweza kuwakinga Watoto wasipatwe na Maambukizi ya VVU kwa asilimi 99.5
Daniel Mwasongwe Mratibu UKIMWI Halmashauri ya Mji Njombe akisoma taarifa ya Kinga ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI toka kwa Mama kwenda kwa Mtoto kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2022 Jumla ya Wajawazito 150 walikuwa tayari wanaishi na maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI na Wajawazito 2727 waliweza kupima Virusi vya UKIMWI Ambapo Kati yao 78 Walikutwa na Maambukizi ya VVU sawa na asilimia 2.9
Aidha, Kwa upande wa Wanaume 2058 waliohudhuria Kliniki ya Wajawazito kufanya huduma ya Upimaji VVU sawa na asilimia 75.5 ya Wanaume walitakiwa kuhudhuria Kliniki ambapo kati yao Wanaume 31 walikutwa na Maambukizi ya VVU sawa na asilimia 1.5
Sambamba na hilo, jumla ya Watoto 197 waliopima kipimo cha Kwanza cha VVU baada ya kuzaliwa ni Mtoto 1 pekee ndio alikutwa na Maambukizi ya VVU sawa na asilimia 0.5 Hii ina maana kwamba Mkakati wa kuzuia Virusi vya UKIMWI toka kwa Mama kwenda kwa Mtoto umeweza kuwakinga Watoto wasipatwe na Maambukizi ya VVU kwa asilimi 99.5
Akitoa taarifa ya matumizi ya dawa za ARV’s Mwasongwe amesema kuwa Jumala ya watu 291 kati ya 16,594 wanaotumia dawa za kufubaza makali ya Virusi vya UKIMWI wameripotiwa kutelekeza dawa jambo ambalo linasababisha kurudisha nyuma mapambano hayo sababu kuu zikitajwa kuwa ni imani za dini wanazoamishwa na Viongozi wa Dini kuwa wamepona.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya kudhibiti UKIMWI Filoteus Mligo amesema kuwa lengo la maadhimisho haya ni kutafakari na kuwakumbuka wenzetu waliopoteza maisha kutokana na ugonjwa huo na hivyo kuweza kutathmini na kuwa na mwelekeo na makusudi ya kutokomeza ugonjwa huo kwa kubaini changamoto na mafanikio na hivyo kuweka mikakati katika kupambana na kupunguza VVU na UKIMWI kwenye jamii zetu.
“Niwapongeze Halmashauri kwa kushirikiana na Wadau kwa kuhakikisha kuwa utekelezaji wa Malengo ya kupambana na UKIMWI ndani ya Halmashauri umefikia katika hatua nzuri. Katika Halmashauri yetu lipo jambo ambalo halifurahishi.Tumekuwa na tabia ya kufanya sherehe za kubwa wakati wa kujengea makaburi jambo hili limekuwa likifanyika kwa kutoa michango na sherehe kubwa lakini wakati tunauguza hatutoi michango kumsaidia mgonjwa mpaka anafariki.Tunafanya sherehe michango mikubwa tunaunda na Kamati na wakati anaumwa hatukumtilia maanani ila leo amefariki tunafanya sherehe ya kujenga makaburi.Utamaduni huu sio mzuri.Pia kunakuwa na miziki,ngoma watu wanacheza na kukesha mpaka asubuhi je hili haliwezi kuchangia UKIMWI?Tuache tabia na mila zisizo na maana katika jamii. Hili si jambo jema kwa jamii na hata mbele ya Mwenyezi Mungu”Alisema Mligo
Katika hatua nyingine Diwani wa Kata ya Ramadhan Nickson Nganyang’e amewataka Wazazi kuhakikisha kuwa Wanakuwa karibu na Watoto wao na kushirikiana katika malezi ya Watoto kwani kumekuwa na matukio makubwa ya Kikatili wanaofanyiwa Watoto ambao hupelekea watoto kuharibiwa Kisaikolojia na wakati mwingine kupata magonjwa ukiwemo UKIMWI.
Baadhi ya Wananchi walioshiriki katika Maadhimisho hayo akiwemo Joseph Fute na Rosemary Athanaely wamesema kuwa ni wkati sasa jamii kuanchana na desturi ambazo hazina maadili katika jamii na pia wale wote waliopo katika matumizi ya dawa za kufubaza maambukizi kurudi na kuendlea na ufuasi wa dawa ili kuendelea kuimarisha kinga zao.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe