Katika jitihada za Serikali kuboresha usimamizi wa ardhi na kuhakikisha wananchi wanamiliki maeneo yao kisheria, Bw.Eligius Wella (Madebe), mkazi na mwekezaji katika kilimo cha parachichi kijiji cha Kifanya, ni miongoni mwa wananchi waliopatiwa hati miliki katika Kliniki ya Ardhi inayoendelea kijijini hapo.
Mwekezaji huyo amekabidhiwa jumla ya hati miliki 16 za maeneo mbalimbali anayoyamiliki na kamishna msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Njombe Bw.Fulgence Kanuti,hatua ambayo imepongezwa kama mfano wa kuigwa kwa wananchi wengine wenye maeneo zaidi ya moja.
Zoezi la utoaji wa hati hizo linafanyika kupitia Kliniki ya Ardhi iliyoandaliwa na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, inayofanyika katika ofisi ya kijiji cha Kifanya, ambapo wananchi wote waliokamilishiwa nyaraka za umiliki wanahamasishwa kufika kuchukua hati zao.
Kliniki inaendelea hadi tarehe 17 Oktoba 2025, na inalenga kuwahudumia wananchi kwa kuwapatia msaada wa kisheria na kitaalamu kuhusu masuala ya umiliki wa ardhi.
Mamlaka ya kijiji kupitia mtemdaji wake Bw.Bariki Kabelege inatoa wito kwa wananchi wote waliotayarishiwa na wanahitaji hati miliki kufika ofisini kabla ya tarehe ya mwisho.
"Miliki ardhi kisheria, epuka migogoro kwa maendeleo endelevu."
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe