Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe.Antony Mtaka amefungua mafunzo ya uwasilishaji ,usambazaji na Uhamasishaji wa matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi kwa waandishi wa Habari wa Mkoa wa Njombe na Ruvuma .
Akifungua kikao hicho Septemba 18 ,2023 mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe.Mtaka amewataka waandishi wa habari kuhakikisha wanatumia mafunzo hayo vizuri ili jamii iweze kupata habari zenye takwimu sahihi
Aidha Mhe Mtaka, amewasihi waandishi wa habari kujiendeleza nakuwa na utamaduni wa kujisomea na kujifuza kutoka kwa watu wengine pamoja na kuongeza ubunifu katika kazi wanazozifanya.
"Mwandishi wa habari mzuri ni mwandishi anayesoma kazi za wengine, ili uwe mshindani lazima uwe msomaji mzuri, Pata muda wakusoma, lazima mtafute maarifa. Dunia ya leo huna ubunifu, huna maarifa wewe umebaki nyuma sana. Tumieni hii fursa vizuri kujifunza"
Katika hatua nyingine amewakumbusha wanahabari nguvu waliyo nayo kwenye kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii endapo wataamua kuitumia kalamu vizuri kwa kuandika taarifa sahihi ambazo zinahusisha utafiti na rejea.
Naye Spika Mstafu wa Jamhuri ya Muungamo wa Tanzania na Kamisa wa Sensa Anna Makinda amesema lengo la mafunzo hayo nikuwajengea uwezo waandishi wa habari katika kuandika na kuripoti habari zinazohusisha takwimu.
"Waandishi wa habari lazima mzingatie taaluma, sisi watu wa takwimu tunataka waandishi wa habari mseme kile kilichopo kwa sababu unaweza kuwa mwandishi wa habari wa porojo tuu na wananchi wakachanganyikiwa "
Amesisistiza kuwa ni vyema wana habari wakafahamau kuwa ni vizuri wakawa na nguvu haswa kwenye masuala ya takwimu na kile watakachokiandika kiweze kuaminika kwenye jamii kwa sababu takwimu ndiyo inayojenga nchi.
Mafunzo hayo kwa wanahabari yanayotolewa na Ofisi ya Takwimu Taifa yanafanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe na yatahitimishwa Tarehe 19 September 2023.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe