Halmashauri ya Mji Njombe tunatarajia kuupokea Mwenge wa Uhuru Tarehe 17 Juni, 2024 katika kata ya Matola kijiji cha Boimanda ukiwa unatoka Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.
Mwenge wa Uhuru ukiwa Mjini Njombe utakimbizwa kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo kwenye kata 6 ambazo ni kata ya Matola utafanyika Uzinduzi wa vyumba 3 na ofisi 1 Shule ya Msingi Boimanda na Uzinduzi wa kikundi cha kwaya kinachohamadisha uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2024, Uwemba utafanyika Ukaguzi wa Msitu wa Asili Isililo, Yakobi utafanyika Ukaguzi wa shamba la parachichi, Mjimwema utafanyika Uzinduzi wa kituo cha mafuta cha Amoil, Njombe Mjini utafanyika Ukaguzi wa kikundi cha vijana SUNJO na ukaguzi wa klabu ya kupinga Rushwa katika shule ya Sekondari Mpechi na katika kata ya Ramadhani utafanyika Uzinduzi wa jengo la mama na mtoto katika hospitali ya Mji Njombe (Kibena).
Baada ya shughuli ya kukimbiza Mwenge wa Uhuru kwenye miradi ya maendeleo , utafanyika mkesha katika viwanja vya stendi ya zamani Njombe Mjini.
Wananchi wote mnakaribishwa kuupokea Mwenge wa Uhuru kwenye miradi iliyopo katika maeneo yenu, kukesha na Mwenge wa uhuru na kuukabidhi Mwenge.
Kauli mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 inasema "Tunza mazingira na shiriki Uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu"
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe