Mkoa wa Njombe leo umefanya uzinduzi rasmi wa kampeni ya Chanjo ya Polio awamu ya tatu ambapo kupitia kampeni hiyo watoto 139,281 wenye umri chini ya miaka mitano wanataraji kuchanjwa ili kujikinga na ugonjwa huo,uzinduzi uliofanyika katika kituo cha Afya Njombe Mjini na unatarajiwa kufanyika kwa muda wa siku nne.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe amesema kuwa katika awamu zilizopita Mkoa wa Njombe uliweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa ambapo katika awamu ya kwanza Mkoa wa Njombe ulichanja kwa asilimia 116 na awamu ya pili asilimia 108.
Dkt. Grace Charles ni Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya Kitengo cha Chanjo ambapo amesema kuwa Njombe ni Miongoni mwa Mikoa ambayo imekua ikifanya vizuri na hii ni kutokana na ushirikiano ambao umekuwa ukiwepo na hivyo amewataka Wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo la chanjo.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Ayubu Mndeme akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Njombe kwenye Uzinduzi huo amesema kuwa chanjo hiyo ni muhimu kwani kwa Mtoto ambaye hajapatiwa chanjo ni hatari kwa maisha yake, wenzake, na jamii inayomzunguka kwani anaweza kuambukiza au kuambukizwa ugonjwa kwa kutokuwa na kinga na hivyo kuwataka wahudumu wa afya kuhakikisha kuwa wanaimarisha usimamizi na utoaji huduma kwa kipindi chote.
"Nitoe rai kwa kwa Wananchi wote kuepuka upotoshaji kuhusiana na chanjo kwani chanjo hii ni ile ile ambayo hutolewa kwenye vituo vya huduma za afya katika ratiba ya kawaida ya chanjo.Ni salama na hutolewa bure hivyo kila mmoja wetu ahakikishe anakuwa mlinzi wa mwenzake."Alisema
Kwa upande wao baadhi ya wazazi ambao watoto wao walibahatika kupatiwa chanjo katika awamu zilizopita na leo hii wameshiriki kwenye uzinduzi huo wamesema kuwa chanjo hiyo ni muhumu kwani itawasaidia katika makuzi yao na hivyo kuwataka wazazi kupokea chanjo hiyo.Alisema Henela Busagala Mkazi wa Ramadhani
Naye Agness Flowin Mkazi wa Njombe Mjini amwashauri wazazi na walezi kuachana na kauli potofu ambazo zinaweza kuhatarisha maisha na makuzi ya watoto wao kutokana na kukosa chanjo hiyo kwa kuwa na imani potofu.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe