• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu na uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mazingira na Usafishaji
      • Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu.
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Election
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Utamaduni,Sanaa na Michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

NJOMBE YAZINDUA MWONGOZO WA ELIMU NA MKAKATI MPYA WA KUTOKOMEZA ZIRO

Tarehe iliyowekwa: September 12th, 2022

Mkoa wa Njombe umezindua mwongozo wa elimu leo na  kuweka mkakati mpya  wa kutokomeza ziro kwa wanafunzi wa kidato cha nne,ambapo walimu wametakiwa kuwafundisha watoto masomo matano wanayoyaweza  badala ya kumi na moja.

Akiwasilisha mkakati huo Mkuu wa Mkoa wa Njombe,Mhe. Anthony Mtaka  katika uzinduzi wa Mwongozo wa elimu uliofanyika  leo shule ya sekondali Mpechi, amesema kuwa badala ya walimu kuendelea kuwafundisha wanafunzi masomo yote hata ambayo hawayawezi ni wakati sasa walimu kuwapima wanafunzi hao ili kutambua masomo matano ambayo kila mwanafunzi anayaweza na kuwafundisha zaidi ili waweze kufaulu vizuri badala ya kuwaongezea mzigo wa masomo mengine ambayo hawayawezi.

Ametoa rai kwa walimu na wanafunzi kuhakikisha wanatokomeza ziro na shule ya Serikali  itayofaulisha na kuingia kumi bora,itapewa milioni tano taslimu kwaajili ya walimu sio matumizi ya shule na mwanafunzi atayefaulu daraja la kwanza la pointi saba atapewa laki tano,mwanafunzi wa kike na wenye mahitaji maalumu wataopata daraja la kwanza la pointi nane na tisa (single digit) watapewa laki tano,Mwalimu atayefaulisha kila alama A atapewa elfu ishirini na alama B atapewa elfu tano.

Amesema kuwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa itatoa fedha hizo kama motisha kwa walimu na wanafunzi,ili mkakati wa kutokomeza ziro ufanikiwe lakini pia wazazi na walezi wa wanafunzi hao wana nafasi kubwa sana katika ufaulu wa wanafunzi hivyo ili mkakati huo ufanikiwe wazazi hawana budi kuhakikisha wanawasimamia watoto wao kujisomea.

Akielezea mikakati iliyopo katika vitabu vitatu vilivyozinduliwa leo Afisa elimu Mkoa wa Njombe,Mwl. Nelasi Mulungu amesema mikakati iliyopo katika vitabu hivyo ni kuhakikisha wanafunzi wote wanaoanza darasa la kwanza wanamaliza darasa la saba,kuhakikisha wanafunzi wote wanapofika  darasa la pili wanajua kusoma,kuandika na kuhesabu na kila mwanafunzi anayeanza kidato cha kwanza anamaliza kidato cha nne.

Mulungu amesema mikakati hiyo inawaelekeza viongozi namna ya kusimamia na kufuatilia  shule katika maeneo yao,huku  ikiwalenga hasa Walimu wakuu,Wakuu wa shule,Maafisa elimu Kata,viongozi ngazi ya Halmashauri na Mikoa.










Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI,UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI. April 25, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UBORESHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA. December 20, 2024
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. April 18, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKUU WA WILAYA NJOMBE MHE. JUMA SWEDA ATOA WITO KUHUSU CHANJO YA PILI YA POLIO.

    April 29, 2025
  • AFISA MWANDIKISHAJI JIMBO LA NJOMBE MJINI AKUTANA NA VYAMA VYA SIASA

    April 24, 2025
  • ZIARA YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YA NJOMBE KUKAGUA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2025

    April 04, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Njombe awaonya wenyeviti kuhusu uharibifu wa miradi ya maendeleo

    February 15, 2025
  • Angalia zote

Video

WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA KUJITUMA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe