• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu na uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mazingira na Usafishaji
      • Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu.
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Election
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Utamaduni,Sanaa na Michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

RC Rubirya Akabidhiwa Vyumba 103 vya Madarasa Wilaya ya Njombe

Tarehe iliyowekwa: December 29th, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhandisi Marwa Rubirya leo amekabidhiwa vyumba 103 vya madarasa katika Wilaya ya Njombe ambavyo vyumba hivyo vimejengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Halmashauri ya Mji  Makambako na Halmashauri ya Mji Njombe ambapo makabidhiano hayo yamefanyika katika Shule ya Sekondari Mpechi kwa kukabidhiwa vyumba 05 vya madarasa ikiwa ni ishara ya makabidhiano hayo Kiwilaya.

Akizungumza wakati akisoma taarifa ya makabidhiano, Mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Gwakisa amesema kuwa katika vyumba 103 vya madarasa vilivyojengwa kwenye Wilaya ya Njombe ujenzi wa vyumba hivyo umekamilika kwa asilimia mia moja na pia vimewekewa samani ikiwa ni viti na meza na amezishukuru kamati za ujenzi kwa namna walivyosimamia miradi hii mpaka kukamilika kwake.

“Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutuletea maendeleo Wananchi wa Tanzania kwa miradi hii mikubwa ya ujenzi wa madarasa. Kipindi cha nyuma tulitumia muda huu kuchangisha wananchi ili kidato cha kwanza waweze kuingia madarasani. Lakini leo hii  tumejengewa madarasa na Wananfunzi wa kidato cha kwanza wote wanaingia darasani pasipo kumsumbua Mwananchi na michango.”Alisema Kissa

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhandisi Marwa Rubirya amepongeza hatua iliyofikiwa  ya ukamilishaji  wa vyumba 103 vya madarasa ambavyo chanzo cha fedha za mradi huo ikiwa ni mapambano dhidi ya UVIKO.

“Pamoja na kazi nzuri tuliyoifanya niwape changamoto katika awamu ya pili ya miradi na hii itakuwa ni sera yetu ya Mkoa  kuhakikisha kuwa tunajenga mazingira mazuri ya kazi kwa Waalimu ikiwa ni pamoja na kuwajengea ofisi nzuri. Kila tunapojenga vyumba viwili vya madarasa lazima tujenge ofisi kwa ajili ya Waalimu.”Alisema Mkuu wa Mkoa

Aliendelea kusema “Bado tunataka kujua jinsi fedha hii ilivyotumika. Tumeandaa fomu maalumu itakayosambazwa kwenye kila shule itakayokuwa na mchanganuo wa gharama za fedha zilizotumika katika kila hatua ya ujenzi  ikiwa ni kuanzia msingi, kupandisha kuta, kuezeka, kupaua na hatua za umaliziaji. Niwapongeze sana Shule ya Sekondari Mpechi kwa hatua hii ya ujenzi. Madarasa ni mazuri na Milango iliyotumika hapa ni ya kiwango cha juu.  Alisema Rubirya.

Aidha Mkuu wa Mkoa ametoa rai kwa wazazi na walezi kuhakikisha kuwa watoto wote waliofaulu kidato cha kwanza kuhakikisha kuwa ifikapo januari 17 watoto wote wanaripoti shuleni kwani madarasa yapo ya kutosha na hakuna sababu ya shule kutoyatumia madarasa mapya kwani yamejngwa kwa sababu hiyo.

Shule ya Sekondari Mpechi ilipatiwa kiasi cha Shilingi milioni 100 ikiwa ni kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 5 vya madarasa na samani ambavyo vimekabidhiwa rasmi leo

                                                                                                                         

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI,UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI. April 25, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UBORESHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA. December 20, 2024
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. April 18, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKUU WA WILAYA NJOMBE MHE. JUMA SWEDA ATOA WITO KUHUSU CHANJO YA PILI YA POLIO.

    April 29, 2025
  • AFISA MWANDIKISHAJI JIMBO LA NJOMBE MJINI AKUTANA NA VYAMA VYA SIASA

    April 24, 2025
  • ZIARA YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YA NJOMBE KUKAGUA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2025

    April 04, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Njombe awaonya wenyeviti kuhusu uharibifu wa miradi ya maendeleo

    February 15, 2025
  • Angalia zote

Video

WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA KUJITUMA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe