Wajumbe wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Mji Njombe wamekubaliana kuongeza nguvu kwenye ufuatiliaji wa madeni ya mikopo inayotolewa kwa vikundi vya wanawake ,vijana na watu wenye ulemavu ili kufuta hoja za madeni ya mfuko wa wanawake ,vijana na watu wenye ulemavu kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Wakizungungumza kwa nyakati tofauti Juni 27,2024 wakati wa kuchangia utekelezaji wa hoja 2.2.2 ya mwaka 2022/2023 inayohusu mikopo iiyotolewa kwa vikundi vya wanawake na vijana ambayo bado haijarejeshwa kwenye Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani kwa ajili ya kujadili Majibu na Utekelezaji wa Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wajumbe hao wameeleza kuwa ,ipo haja kwa Waheshimiwa Madiwani kushirikiana na wataalamu kufuatilia madeni hayo kwa vikundi kwa kuwa vikundi hivyo vinafahamika na vipo kwenye kata wanazozihudumia hivyo ni rahisi kwao kuwahimiza walengwa kufanya marejesho.
Aidha wamekubaliana kuwa taarifa ya marejesho ya mikopo iwe ni sehemu ya taarifa ya utekelezaji wa shughuli za kata inayowasilishwa kila robo ili kuweza kujadili changamoto kurahisisha ufuatiliaji wa mikopo chechefu.
Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe kupitia idara ya maendeleo ya jamii inatoa wito kwa vikundi vyote vilivyopitiliza muda wake wa marejesho ya mikopo, kufanya marejesho ili fedha hizo ziweze kutumika kuwasaidia wahitaji wengine kwa maendeleo ya uchumi wa Taifa.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe