Wafanyabiashara Mjini Njombe wametakiwa kutimiza wajibu wao wakutoa risiti baada huduma ili kuchangia mapato kwa maendeleo.
Kauli hiyo imetolewa Septemba 11, 2023 na Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyaiashara Taifa Ndugu Hamisi Livembe, kwenye mkutano na Jumuiya ya wafanyabiashara Mjini Njombe.
Livembe amesema Jumuiya imekuwa ikipokea kero kutoka kwa wafanyabiashara nakuziwasilisha kwa serikali lakini wafanyabiasha wamesahau wajibu wao wakutoa risiti halali jambo ambalo linapunguza mapato kwa serikali.
Amesisitiza kuwa ni vyema wafanyabiashara wakatambua kuwa haki huambatana na wajibu.
"Unapodai haki kumbuka kutimiza wajibu wako, wafanyabiashara mmejisahau baada ya kero zenu kusikilizwa na kufanyiwa kazi mmeacha kutoa risiti na hapa mnatuangusha maana inaonekana wazi mapato yameshuka na kwamba hampo tayari kutii sheria bila shuruti"
Ili kushughulikia changamoto hiyo amesema jumuiya imeandaa utaratibu wa kuwabaini wafanyabiashara ambao hawatoi risiti.
"Tumeandaa utaratibu na tutakuwa na kikosi maalamu ambacho kitapita nakukagagua machine kwa meizi kadhaa na hapa tutawagundua tuu na tutahakikisha mnawajibika ili serikali isipoteze mapato."
Kwa upande wake meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Njombe Specioza Mickness Owure amewaonya wafanyabiasha wa mazao ya misitu mkoani Njombe ambao wanatabia yakununua risiti feki.
Amesema tayari wamebaini njia zinazotumika na watachukuliwa hatua, ameeliza kuwa ni vyema wafanyabiashara wakafahamu kuwa hakuna nchi inayoendeshwa bila mapato hivyo kutokulipa kodi ni kosa kisheria na nikukosa uzalendo na nchi haiwezi kuwa na maendeleo.
Aidha ametoa tahadhari kwa wananchi kutunza taarifa zao ikiwemo vitambulisho vyao vya taifa (NIDA) ili visitumiwe vibaya kufanya udanganyifu kwenye masuala kodi.
"Wapo watu wamekuwa wanatumia namba za nida za watu, anakufata mtu anakuomba namba yako ya nida au kitambulisho unampatia kumbe anania ovu yakutengeneza namba ya mlipa kodi TIN kwa ajili yakutolea risiti feki jambo ambalo linaweza kukuingiza kwenye matatizo bila kufahamu,kuweni makini usitoe namba au kitambulisho chako bila kufahamu kinatumika kwa kazi gani."
Uongozi wa Jumuiya ya wafanyabiasha Tanzania unafanya ziara mikoa mbalimbali kwa lengo la kuangalia utulivu wa wafanyabiashara na kusikiliza kero mpya kutoka kwa wafanyabiashara ili ziweze kuwasilishwa kwenye mamlaka husika nakupatiwa ufumbuzi , pia kutoa majibu ya baadhi ya kero ambazo ziliwalishwa kupitia kamati maalumu iliyoundwa na Mhe Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambazo tayari zimepatiwa majibu.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe