Kitengo cha Ardhi na Mipango Miji kutoka Halmashauri ya Mji Njombe kimetekeleza zoezi la ugawaji wa hati miliki 58 kwa wakazi wa Mtaa wa Kambarage, Njombe Mjini, ikiwa ni hatua muhimu ya kuimarisha umiliki halali wa ardhi miongoni mwa wananchi.
Akizungumza Julai 23, 2025 wakati wa tukio hilo, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ardhi na Mipango Miji, Halmashauri ya Mji Njombe, Emmanuel Luhamba aliwahimiza wanufaika wa hati hizo
kuhakikisha wanazitunza vizuri kwa kuepuka kuzihifadhi kwenye maeneo yenye unyevu au mazingira yanayoweza kuharibu nyaraka hizo muhimu.
“Hati hizi ni nyaraka za kisheria ,zinathibitisha uhalali wa umiliki wa ardhi ,tunawasihi mzihifadhi sehemu salama na epukeni kuziwekea kwenye unyevu au mazingira hatarishi,” alisema Emmanuel Luhamba
Aidha,akiendelea kuzungumza aliwahimiza wakazi ambao bado hawajapata hati zao kuendelea kufuatilia mchakato huo kwa karibu, kutokana na kuwa hati miliki ni nyenzo muhimu katika kulinda haki ya ardhi na kuondoa migogoro ya umiliki.
“Kwa wale ambao bado hawajapata, mnaombwa kuendelea kufuatilia kwa sababu hati inakupa ulinzi wa kisheria na
kukuwezesha kutumia ardhi yako bila bugudha yoyote,” Alisema Amos Luhamba
, Nao wananchi wa mtaa huo wakiongozwa na Kheri Nyagawa wameipongeza serikali kwa jitihada zake za kuwasaidia kapatiwa hati jambo ambalo litawasaidia katika maendeleo mbalimbali kama vile kupata mikopo kutoka taasisi za kifedha na kupanga vizuri matumizi ya ardhi zao paspo changamoto.
Zoezi la ugawaji wa hati miliki ni sehemu ya mpango wa halmashauri ya mji Njombe ya kuhakikisha kila mwananchi anamiliki ardhi kwa mujibu wa sheria, huku likilenga kupunguza migogoro ya ardhi inayoweza kujitokeza kutokana na kutokuwa na hati rasmi za umiliki.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe