Wananchi wa kata ya Utalingolo Halmashauri ya mji wa Njombe wamepatiwa elimu ya uchaguzi waserikali za mitaa kutoka kwa maafisa uchaguzi wasiadizi wa kata na vijiji kwa kushirikiana na diwani wa kata hiyo Mhe.Erasto Mpete ambaye pia ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe .
Kata ya Utalingolo imekuwa kata ya kwanza kufikisha elimu hiyo mhimu kwa wananchi mabapo vijiji vyote vitatu vya kata hiyo vimefikiwa na wananchi kupata fursa ya kuuliza maswali katika mikutano iliyofanyika kwa siku mbili ambapo kijiji cha ihalula maafisa uchaguzi hao wametoa elimu katika kitongoji cha Nole.
Afisa msaidizi wa uchaguzi kata ya Utalingolo bwana Lenatus Mgani ambaye pia ni mtendaji wa kata Hiyo amewataka wananchi kujitokeza kujiandikisha katika daftari maalumu amabapo uandikishaji utafanyika katika maeneo ya vitongoji wakiwa na vitambulisho vya aina mbalimbali ikiwemo vitambulisho vya nida
Ameanisha pia sifa za mpiga kura anayefika kujiandikisha katika fatari Maalumu la mpiga kura kuwa ni pamoja na kua raia wa Tanzania,Awe mkazi wa kitongoji husika awe na akili timamu mtu mwenye kipato awe na akili timamu na awe na umri wa kuanzia mika 18 na kuendelea
Katika hatua nyingine wananchi pia wamehamasishwa kujitokeza kugombea nafasi za uenyekiti wa kijiji ,uenyekiti wa kitongoji na ujumbe wa serikali ya halmashauri ya kijiji ambapo pia amebainisha sifa za anayetaka kuchaguliwa kua ni awe raia wa tanzania, awe na umri kuanzia miaka 21 na kuendelea, ajue kusoma na kuandika kiswahili au kingereza kwa ufasaha, awe na kipato halali cha kumuwezesha kuishi,aweni ni mkazi wa eneo husika, awe na akili timamu na awe mwanachama wa chama cha siasa,awe na akili timamu na awe amejiandikisha katika daftari maalumu la mpiga kura.
Amesema kuwa uchaguzi serikali za mitaa utafanyika hapo tarehe 27 mwezi Novemba ambapo wagombea watafanya kampeni za kujinadi kwa wapiga kura kwa muda wa siku sita Ambapo amewaomba wananchi kushiriki katika uchaguzi huo wa serikali za mita kwa amani na utulivu.
Diwani wa kata ya utalingolo ambaye pia ni mwenyekiti wa Halmashauri ya mji Njombe Mhe.Erasto Mpete akizungungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vya kata ya utalingolo amewataka kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari maalumu la mpiga kura na Sanjari na kuhakikisha wanawasikiliza na kuwaelewa wagombea na kisha kujitokeza kwa wingi kupiga kura hapo novemba 27 mwaka 2024 kwenye vituo vya kupigia kura ambavyo vitakuwa katika maeneo yao ya viongoji.
Amewataka wananchi kuwachagua viongozi wenye sifa njema wenye kujitolea katika shughuli mbalimbali za maendeleo na za kijamii ili waweze kuwaletea maendeleo katika nyanja mbalimbali.
Baadhi ya ananchi akiwemo vitalia mwajombe kutoka kijiji cha Ihalula na Grace Mpete kutoka kijiji cha Utalingolo wameishukuru serikali hususani viongozi wa kata hiyo wakiongozwa na diwani wa kata hiyo Erasto Mpete ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa njombe kwa kuwahisha elimu hiyo ya uchaguzi.
‘’Sisi wananchi hii elimu ya uchaguzi tumeipokea vizuri na tunashukuru Serikali kutufikia kwa upande wangu niko tayari kugombea na kuwapigia kura watakaogombea’’anabaisha Vitalia Mwajombe mkazi wa kijiji cha Ihalula.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe