Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mheshimiwa Kissa Gwakisa Kasongwa amewataka Wananchi wa Kijiji cha Boimanda Kata ya Matola kuacha habari za upotoshaji juu ya matumizi ya chanjo ya UVIKO 19 ambapo Wananchi wengi wamekuwa na imani potofu juu ya matumizi ya chanjo hiyo.Akizungumza wakati wa ziara yake katika Kijiji cha Boimanda Kata ya Matola Halmashauri ya Mji Njombe
Mheshimiwa Kissa amewataka Wananchi kupuuza habari za mitandao na za uzushi kuwa chanjo ya UVIKO inaleta madhara kwenye afya na kupelekea kifo na pia kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.“Ingekuwa chanjo ya UVIKO Inamadhara basi Mheshimiwa Rais angekuwa wa kwanza kupata madhara hayo kwani ndiye aliyeongoza zoezi la utoaji chanjo.Mimi mwenyewe nimechanja na mpaka sasa bado nipo vizuri.Tungetaka kuuliwa tungeweza kuuliwa kwa njia mbalimbali,yapo mambo mengi tunapokea kutoka nje ya nchi.Na huduma ya chanjo haijaanza leo ni huduma ya siku nyingi.Ukiona mtu anaongea maneno ya uongo juu ya chanjo basi huyo ujue hayajamkuta. Tujitokeze kuchanja, Chanjo ni salama na ni kwa ajili ya uhai wetu.”Alisema Mkuu wa Wilaya.
Wakizungumza mara baada ya kusikiliza elimu ya chanjo waliyopatiwa kutoka kwa Mkuu wa Wilaya baadhi ya Wananchi kutoka katika Kata ya Matola Kijiji cha Boimanda wameshukuru ziara hiyo ya Mkuu wa Wilaya kwani imewapa hamasa kwao kushiriki zoezi la chanjo kwani uelewa juu ya uchanjaji ulikuwa ni mdogo.Winfrida Joseph Mgaya na Elizabeth John ni wakazi wa Kijiji cha Boimanda ambao kwa pamoja wanamshukuru Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya kwa elimu hiyo ambayo iliwapelekea kupatiwa huduma ya chanjo.“Mwanzoni nilikua sielewi maana walisema kuwa chanjo zinamadhara na wakati mwingine zinaweza kusababisha kifo lakini nashukuru leo nimepata elimu na nimechanja. Nawashauri wenzangu ambao bado hawajachanja kuhakikisha kuwa wanachanja”Alisema Elizabeth.
Licha ya kutoa elimu ya chanjo na kutoa jumbe kuu za Serikali ikiwa ni Pamoja na suala la sensa na mbolea Mkuu wa Wilaya pia amebahatika kutembelea katika shule ya Msingi Boimanda na kujionea hali halisi ya madarsasa ambapo ameshauri kuwa Halmashauri ione ni kwa namna gani inaweza kutenga fedha kupitia zidio la makusanyo ili kujenga vyumba vipya vya madarasa katika shule hiyo kutokana na uchakavu uliopo katika shule hiyo kwa sasa.Ikumbukwe kuwa Mkuu wa Wilaya ya Njombe anaendelea na ziara yake ya kutembelea katika kila kijiji kuzungumza na wananchi na kutatua kero mbalimbali ambapo kwa leo yupo katika Katt ya Matola Halmashauri ya Mji Njombe.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe