Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi Bi.Lucy Saleko,Oktoba 10,2025, ameongoza zoezi la kugawa hati miliki kwa Wananchi wa Kata ya Kifanya kwenye kliniki ya Ardhi inayoendelea.
Kliniki hiyo inayoendeshwa na Wizara ya Ardhi kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe inaendelea katika ofisi ya kijiji cha Kifanya na inatarajiwa kukamilika tarehe 17 Oktoba 2025.
Jumla ya hati miliki 229 zimeandaliwa na kukamilika kwa ajili ya kugawiwa wananchi, hatua inayolenga kuimarisha umiliki halali wa ardhi nakuepuka migogoro ya isiyo ya lazima.
"Miliki Ardhi kisheria ,epuka migogoro ya ardhi kwa maendeleo endelevu".
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe