Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, Juni 12,2024 alifanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Mji Njombe na kueleza kuridhishwa na hatua zilizofikiwa kwenye miradi hiyo muhimu ya sekta ya elimu. Katika ziara hiyo, Mhe. Mtaka alitembelea ujenzi wa jengo la gorofa lenye vyumba 8 vya madarasa na ofisi 4 za walimu na matundu 4 ya vyoo katika Shule ya Sekondari Uwemba, mradi uliokadiriwa kugharimu zaidi ya shilingi milioni 600 hadi kukamilika.Pia alikagua ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Wikichi unaotekelezwa kupitia programu ya SEQUIP kwa gharama ya shilingi milioni 583.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe