Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe.Juma Sweda Juni 18,2025 alifanya ziara Halmashauri ya Mji Njombe na kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa matundu ya vyoo na mabweni katika shule ya Sekondari Matola,miradi inayotekelzwa kwa fedha zaidi ya Milioni 280 kutoka serikali kuu na mapato ya ndani ya Halmashauri.Katika ziara hiyo alipongeza juhudi zinazofanywa na Serikali kwa kutoa fedha zinazotumika kuboresha miundombinu mbalimbali kwenye sekta ya elimu na afya jambo ambalo linaondoa usumbufu kwa wananchi kuchangia shughuli za maendeleo.Katika kipindi cha miaka 5 ,zaidi ya shilingi Bilioni 1.5 zimetumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kata ya Matola katika sekta ya Elimu na Afya.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe.Anthony Mtaka akizungumza kwenye Baraza maalumu la kujadili hoja za mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) Juni 16,2025 pamoja na mambo mengine ametoa wito kwa Halmashauri ya mji Njombe kuchangamkia fursa za uwekezaji hata nje ya Halmashauri ili kuuendelea kuinua hadhi yake yakuwa makao makuu ya Mkoa wa Njombe.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe.Anthony Mtaka ametoa pongezi kwa waheshimiwa madiwani ambao wanamaliza kipindi chao cha uongozi baada ya miaka mitano akiwasisisitiza kutembea kifua mbele kwa kuwa kazi kubwa iliyofanywa na serikali kwenye maeneo yao imefanyika kipindi cha uongozi wao,hivyo wayaseme mafanikio hayo kwa wananchi.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe