Kushirikisha wadau tofauti katika maeneo husika ili kuongeza uchangiaji wa mawazo na/au nyenzo, usimamizi, uratibu na utekelezaji wa kazi za Tume za kudhibiti UKIMWI
Kusimamia uundaji wa Kamati zote za kudhibiti UKIMWI
Kupendekeza na kuchambua hali ya UKIMWI / Mipango na utekelezaji wake na kufikisha katika ngazi husuka kwa hatua zaidi
Kutathmini hali ya UKIMWI katika eneo lake
Kutambua idadi ya waathirika, wagonjwa, yatima na wajane,
Kufanya tathmini ya Kasi ya maambukizi
Kufanya utambuzi wa Mazingira maalum yanayochangia maambukizo