Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji inashughulikia upangaji na uratibu wa mipango ya maendeleo katika miaka husika, usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo ya Halmashauri, Tafiti na ukusanyaji wa Takwimu pamoja na kuratibu shughuli za Uwekezaji. Idara hii inaongozwa na Mchumi wa Mji na imegawanyika katika sehemu tano kama ifuatavyo:-
Kusimamia Uandaaji wa mpango wa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi kila mwaka.
Kuratibu ufanisi wa mifuko ya Halmashauri: LGCDG, Mfuko wa Jimbo na fedha za mapato ya ndani.
Uratibu na utayarishaji wa Mipango shirikishi katika Kata zote za Halmashauri kupitia Mfumo wa O&OD.
Uratibu na utayarishaji wa Mpango na Bajeti ya kila mwaka ya Halmashauri.
Kusimamia uandaaji wa mipango kazi (Action Plans) ya bajeti za kila mwaka na kuziwasilisha katika ngazi husika.
Kuratibu uandaaji wa maandiko ya miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kuratibu maandalizi na utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa sasa (BRN)
Kuratibu maandalizi ya Sera na Mpango Mkakati wa Halmashauri
Kuratibu uandaaji wa taarifa mbalimbali za Halmashauri pamoja na taarifa za utekelezaji wa maagizo kutoka mamlaka za juu za serikali
Kufuatilia utekelezaji halisi na matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo
Kuratibu miradi ya jumuiya za wananchi na taasisi nyinginezo za ndani na nje ikiwemo miradi ya wahisani
Kuratibu utekelezaji wa Mipango ya muda mrefu, kati na mfupi ikiwepo Ilani ya Uchaguzi na uandaaji wa taarifa za utekelezaji wa mipango hiyo
Kuratibu utekelezaji wa mipango shirikishi.
Kuandaa taarifa za Miradi ya maendeleo ya Halmashauri kwa vipindi mbalimbali na kuziwasilisha kwenye mamlaka husika.
Kuandaa mapitio ya bajeti ya kila mwaka baada ya kipindi cha nusu mwaka
Kuandaa mapendekezo ya kubadili matumizi ya vifungu vya bajeti ya maendeleo kila inapobidi.
Kuandaa taarifa za matukio ya kila mwezi na kuiwasilisha ngazi ya mkoa.
Kuhuisha na kuboresha Takwimu za Kiuchumi na Kijamii (Profile) za Halmashauri.
Kuratibu na kuhifadhi takwimu za Idadi ya watu za Halmashauri kwa kutumia rejista za wakazi wa Mitaa na Vijiji
Kuratibu na kutathmini utekelezaji wa Mpango mkakati wa Halmashauri 2012/13 – 2016/17
Kuratibu zoezi la Sensa ya Watu na Makazi.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe