MADAWATI NA MAJUKUMU NDANI YA IDARA YA MAENDELEO YA JAMII
Dawati hili litakuwa na wajibu wa kuratibu, kufuatilia na kutoa taarifa kuhusu ushirikishwaji jamii katika utatuzi wa changamoto za maendeleo ikiwemo uibuaji wa mipango na miradi inayozingatia vipaumbele vya jamii na Taifa. Vilevile litaratibu ukusanyaji na uchambuzi wa takwimu za kijamii na kiuchumi zitakazotumika katika maandalizi ya mipango shirikishi. Dawati hili pia litahakikisha Sera ya Maendeleo ya Jamii ya Mwaka 1996 inatafsiriwa kwa vitendo ngazi ya jamii ili kuwa na jamii na taifa linalojitegemea.
Majukumu ya Dawati
Dawati la litahusika na Kusimamia, kuratibu na kufuatilia:
Ushirikishaji jamii kutambua fursa na vikwazo kwa maendeleo ili kupendekeza njia sahihi ya kutatua kwa kufanya utafiti wa kawaida na utafiti shirikishi;
Ukusanyaji na uchambuzi wa takwimu za uchumi na kijamii na za mchanganuo wa jinsia zitakazotumika wakati wa kutoa maamuzi na upangaji mipango na bajeti, ufuatiliaji na tathmini;
Uhamasishaji wa jamii katika kuandaa au kuhuisha mipango shirikishi na bajeti ya mwaka kwa kuzingatia vipaumbele;
Mafunzo ya Halmashauri za vijiji na Kamati za Mitaa katika utawala bora, maandalizi ya mipango shirikishi na bajeti;
Ushiriki wa jamii katika kuanzisha, kutekeleza na kusimamia miradi ya jamiii na shughuli za kujitegemea kwa kutumia rasimali zilizopo kwenye jamii na kutoka nje;
Uandaaji na usambazaji wa jumbe rahisi zinazoelimisha jamii kuhusu Mikataba ya Kimataifa, Sera na dhana mbalimbali za maendeleo na maelekezo ya Serikali Mfano Tanzania ya viwanda, Ugatuaji Madaraka, Elimu Bure, Mabadiliko ya Tabia Nchi n.k.;
Kuandaa ujumbe rahisi wa kuelimisha jamii kuwa na mtizamo chanya kwenye miradi mikubwa ya Kitaifa ya Gesi, Umeme, Maji, Hifadhi ya Mazingira, Reli na Barabara na fursa zilizopo kwao kwenye miradi hiyo ikiwemo ajira na masoko ya bidhaa wanazozalisha;
Kuratibu shughuli za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF); na
Kutoa Taarifa kwa Mkuu wa Idara.
Dawati hili litahusika na kusimamia, kuratibu na kufuatilia uingizwaji wa masuala ya jinsia katika program, mipango na afua mbali mbali za maendeleo katika ngazi ya Halmashauri. Kimsingi dawati litahakikisha Mikataba na Itifaki za Kimataifa iliyoridhiwa na Nchi na kusainiwa kuhusu Haki za Wanawake na Sera ya Wanawake na Maendeleo ya Jinsia ya Mwaka 2000 zinatafriwa kwa vitendo katika ngazi ya jamii.
Majukumu ya Dawati
Kuhakikisha kuwa masuala ya jinsia katika Halmashauri yanatambuliwa kwa kufanya uchambuzi wa jinsia (gender analysis);
Kuhakikisha masuala ya jinsia yanaingizwa katika mipango ya vijiji, Mitaa na Halmashauri;
Kujenga uelewa miongoni mwa wakuu wa idara, wakuu wa vitengo na madiwani juu ya umuhimu wa kufanyia kazi mapengo ya jinsia ili kuleta haki na usawa wa kijinsia;
Kuratibu kazi za wawakilishi wa masuala ya jinsia katika Halmashauri na Taasisi za Serikali na Wadau;
Kuratibu ukusanyaji wa takwimu za mchanganuo wa kijinsia (Gender Disaggregated Data);
Kuratibu uingizwaji wa masuala ya jinsia katika mipango na bajeti ya Halmashauri;
Kuwezesha mafunzo mbali mbali ya jinsia kwa kadri ya mahitaji;
Kutoa rufaa kwa wahanga wa ukatili wa jinsia (Ustawi wa Jamii, Polisi, Wanasheria na Hospitali);
Kufanya ukaguzi shirikishi wa masuala ya jinsia (participatory gender audit);
Kuitisha vikao vya uratibu wa wadau wa jinsia;
Mikataba ya Kimataifa, Sera, Mikakati na Miongozo ya Jinsia inatafsiriwa kwa vitendo kwa jamii na wadau;
Kuratibu na kusimamia jitihada za kuzuia ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya Wanawake katika ngazi ya Halmashauri na Jamii;
Kutoa Taarifa kwa Mkuu wa Idara; na
Kujenga uwezo wa jamii kutoa nafasi ya ushiriki sawa katika nafasi za uongozi na utoaji wa maamuzi.
Dawati hili litahusika na kusimamia, kuratibu utekelezaji wa Haki, utoaji wa Elimu ya malezi katika ngazi ya familia na maendeleo ya ujumla kwa mtoto. Kimsingi dawati hili litatekeleza Afua zinahusu Haki na Maendeleo ya Mtoto kama zilivyoainishwa katika Sera, Sheria na Mikataba ya Kikanda na Kimataifa inayohusu masuala ya watoto iliyoridhiwa na kusainiwa na serikali. Aidha dawati litajikita katika kuzuia vitendo vyote vinavyosababisha madhara na mmomonyoko wa maadili kwa mtoto. Dawati litahakikisha Sera ya Maendeleo ya Mtoto 2008 na Sheria ya Mtoto Na. 21 ya Mwaka 2009 vinatafsiriwa kwa vitendo ngazi ya jamii.
Majukumu ya Dawati
Kuratibu program za haki na Maendeleo ya Mtoto zinazotekelezwa na wadau ili kuhakikisha zinafuata Sera, Sheria za Serikali na Mikataba ya Kikanda na Kimataifa iliyolenga Haki za Mtoto;
Kuhamasisha na Kuelimisha familia, jamii na wadau katika kuwekeza kwenye malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto ili kuwa na jamii bora iliyojengwa kwa misingi ya umoja na mshikamano wa kitaifa;
Kuunganisha nguvu za wadau mbali mbali wanaofanya kazi za watoto ili kuepusha migongano na matumizi mabaya ya rasilimali fedha na watu;
Kuhakikisha ukatili dhidi ya watoto unatokomezwa kupitia mipango na program za kitaifa ambazo zimeandaliwa kwa kushirikiana na wadau;
Kuongeza uelewa wa jamii kuhusu masuala ya haki, ulinzi na ustawi wa mtoto kupitia uelimishaji umma kwa kutumia vipindi vya redio za jamii, runinga, maadhimisho, mikutano na midahalo;
Kuratibu ukusanyaji, uhuishwaji, uchambuzi na usambazaji wa takwimu zinazohusu watoto;
Kuratibu uanzishwaji na uendeshaji wa mabaraza ya watoto katika ngazi ya kijiji, Kata, na Wilaya;
Kuratibu uanzishwaji na uendeshwaji wa vikundi vya malezi kwa familia katika ngazi ya jamii;
Kuanzisha na kufuatilia matumizi ya rejista ya matukioa ya uvunjifu wa haki za watoto na namna yalivyoshughulikiwa katika ngazi ya kijiji, Kata na Halmashauri; na
Kutoa taarifa kwa Mkuu wa Idara.
Kulingana na Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na.24 kama ilivyorekebishwa Mwaka 2005, Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii, nchini wameteuliwa na kutumika kama Wasajili Wasaidizi katika ngazi za Mkoa, Wilaya/Mji. Hivyo Majukumu ya Dawati la NGOs yameanishwa kwa Mujibu Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali. Dawati litahakikisha Sera ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya Mwaka 2001 inatafsiriwa kwa vitendo na wadau wanaofanya kazi ngazi ya jamii na jamii yenyewe.
Majukumu ya Dawati
Kuwezesha Usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yaliyopo katika maeneo husika;
Kuratibu shughuli za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yaliyopo katika eneo husika;
Kufuatilia shughuli, miradi na program zinazotekelezwa na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ili kubaini kama zinawafikia na kuwanufaisha walengwa;
Kuandaa taarifa kuhusu Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Yaliyopo Katika Eneo lake na kuwaikilisha kwa Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali;
Kuratibu Uwasilishaji wa mpango kazi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na kuingiza/kuhuisha katika mipango na bajeti za Wilaya/Miji au Mikoa husika;
Kutatua changamoto mbali mbali ikiwemo migogoro zinazoyakabili Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yaliyo ndani ya eneo husika;
Kuwezesha utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali 2001, Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na.24/2002 kama ilivyorekebishwa mwaka 2005 na Kanuni mbali mbali za usajili na uratibu wa Mashirika haya nchini;
Kutoa ushauri wa wadau kuhusu usajili, ufuatiliaji na uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kwa Mashirika na wadau mbali mbali kwenye eneo husika;
Kuwezesha na kukuza ushirikiano kati ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini, Serikali na wadau mbali mbali wa maendeleo;
Kusimamia uanzishaji na utendaji wa Kamati za Usimamizi wa Kanuni za Maadili za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ndani ya Wilaya kwa lengo la kukuza uwazi na uwajibikaji miongoni mwa Mashirika haya kwa jamii inayohudumiwa;
Kusimamia chaguzi za viongozi wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika ngazi husika;
Kuhamasisha uanzishaji wa mitandao ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika ngazi ya eneo husika kwa lengo la kukuza na kuimarisha ushirikiano miongono mwa mashirika haya;
Uratibu wa Vikundi vya maendeleo vya Kijamii (CBOs);
Kuratibu Watoa huduma za Msaada wa Kisheria katika Jamii; na
Kutoa taarifa kwa Mkuu wa Idara.
Masuala mtambuka ni mikakati ya kitaifa inayogusa jamii na kupaswa kutekelezwa na kila sekta na kuitolea taarifa ya utekelezaji. Mikakati hiyo ni pamoja na ule wa UKIMWI, Lishe, Mazingira, Afya. Wataalam wa Maendeleo ya Jamii kwenye ngazi ya Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri wanalo jukumu la kusimamia na kuratibu masuala mtambuka kwa mujibu wa miongozo au maandiko na maelekezo ya utekelezaji wa mikakati hiyo. Masuala mtambuka yatakayoratibiwa na dawati hili ni pamoja na UKIMWI, Usajili wa Vizazi na Vifo ngazi ya jamii, lishe, Mazingira na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (CHF).
Kwa mujibu wa Mwongozo wa Utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NMSFEE) wa Mwaka 2016, Mratibu wa Dawati la Uwezeshaji Wananchi ni Afisa Maendeleo ya Jamii. Dhumuni kubwa la Mwongozo huu ni kumuwezesha mwananchi kiuchumi ili kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla. Ili kufanikisha azma hii ya sarikali ni muhimu kuwepo kwa Dawati litakaloratibu Kazi hiyo.
Majukumu ya Dawati.
Kushirikiana na Kamati ya Uwezeshaji ya Hamashauri kutekeleza Mkakati wa Uwezeshaji wananchi kiuchumi;
Kuhamasisha wananchi kujiunga na SACCOS na VICOBA kwa lengo la kujiwekea akiba na kupata mitaji;
Kuchambua fursa zilizoko katika Miradi mikubwa ya uwekezaji na miradi ya Kitaifa na kuelimisha wazawa ili waweze kushiriki/kuajiriwa;
Kuratibu Mfuko wa Maendeleo ya wanawake WDFkatika ngazi ya Halmashauri;
Kuratibu utoaji wa mikopo inayotokana na asilimia 10% ya mapato ya ndani ya Halmashauri kwa ajili ya kuwezesha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu;
Kuratibu Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake katika Halmashauri;
Kuhakikisha Halmashauri inatenga maeneo maalum ya uwekezaji kiuchumi kama vile kilimo, viwanda na biashara ndogondogo na za kati; na
Kufuatilia utekelezaji wa shughuli za uwekezaji kiuchumi katika
SHUGHULI ZINAZOTEKELEZWA NA PROGRAM YA UKIMWI
SHUGHULI ZINAZOTEKELEZWA NA DAWATI LA UWEZESHAJI WANACHI KIUCHUMI
MAJUKUMU YA KITENGO CHA VIJANA
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe