Idara ya Mipangomiji na Ardhi hushughulikia masuala mbalimbali kuhusu uendelezaji wa Makazi, Ardhi na Maliasili. Idara hii inatekeleza na kusimamia Program mbalimbali zinazohusiana na maendeleo ya makazi ikiwemo Program ya kuboresha miundombinu ya jamii katika maeneo yasiyopangwa (DMDP), Program ya Mtandao wa Miji Tanzania (TACINE).
Muundo wa Idara
Idara ya Mipangomiji na Ardhi ni mojawapo kati ya Idara 19 za Halmashauri zinazofanya kazi chini ya Mkurugenzi wa Halmashauri. Idara imegawanyika katika sehemu nne zinazojumuisha Miliki na Maendeleo ya ardhi, Mipango ya Makazi, Uthamini, Upimaji na Ramani.
Kuandaana kusimamia utekelezaji mipango ya uendelezaji wa ardhi katika Halmashauri kwa kuzingatia Mpango Kabambe, Sheria ya Mipangomiji Sura Na. 8 ya mwaka 2007, sheria ya Ardhi na 4 ya mwaka 1999 nakanuzi zake pamoja na mingozo mingine inayotolewa na Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
i. Mradi wa kuboresha miundo mbinu kwenye maeneo yasipangwa (DMDP)
ii. Usimamiaji na utunzaji wa takwimu za kijiografia (GIS)
iii. Kutambua na kutoa haki miliki katika maeneo yasiyopimwa (Leseni za Makazi)
iv. Kuratibu Program ya Mtandao wa Miji Tanzania (TACINE)
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe