Agosti 8, 2025 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Charles Makongoro Nyerere, amewataka wakuu wa mikoa na wilaya nchini kuhakikisha wanahimiza lishe bora kwa wananchi, kuhamasisha utaratibu wa kuweka akiba ya mazao, na kusimamia ipasavyo miongozo ya wizara ikiwemo maandalizi ya maonesho katika maeneo yao.
Akizungumza katika hotuba yake jijini Mbeya wakati akifunga maonesho ya Nanenane katika Viwanja vya John Mwakangale, Mhe Makongoro ambaye alikuwa mgeni rasmi wa tukio hilo alisema hatua hizo ni muhimu katika kuhakikisha ustawi wa wananchi katika lishe bora kutokana na mikoa ya nyanda za juu kuongoza katika udumavu pamoja na kupunguza changamoto za upungufu wa chakula.
“Tunapaswa kuendelea kuhamasisha lishe bora kwa familia zetu na kuhakikisha tunahifadhi akiba ya chakula cha kutosha na kufuata kikamilifu miongozo inayotolewa na wizara husika,” alisema Mhe. Makongoro Nyerere.
Akiendelea kutoa huba yake aliongeza kuwa maonesho ya Nanenane yamekuwa jukwaa muhimu la kuonesha teknolojia mpya za kilimo, ufugaji, na uhifadhi wa chakula, na akawataka viongozi wa mikoa yote kutumia fursa hiyo kuwaelimisha wananchi.
Maonesho ya mwaka huu yaliwakutanisha wakulima, wafugaji, watafiti, wajasiriamali na taasisi mbalimbali kutoka nyanda za juu kusini kwalengo la kuongeza tija na thamani ya mazao ya kilimo.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe