Mafunzo kwa watendaji wa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29,2025 ambao ni makarani waongozaji wapiga kura 366 yamefanyika leo Oktoba 25, 2025 katika Jimbo la Njombe Mjini.
Mafunzo hayo yalifunguliwa rasmi na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Njombe Mjini Bw. Samson Medda ambaye pia aliwaapisha washiriki hao na kusimamia zoezi la kutoa tamko la kujitoa uanachama wa vyama vya siasa pamoja na kuapa kiapo cha kutunza siri za kazi zao.
Katika mafunzo hayo, makarani wamepatiwa elimu kuhusu wajibu na majukumu yao katika siku ya kupiga kura, ikiwemo namna bora ya kuwapokea na kuwaongoza wapiga kura kwenye vituo vya kupigia kura, kuhakikisha taratibu zinafuatwa, na kudumisha usiri wa mchakato wa uchaguzi.
Msimamizi wa Uchaguzi amewasisitiza makarani hao kufanya kazi kwa uadilifu, kutenda haki kwa kila mpiga kura na kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia viapo walivyoapa.
Aidha,amewakumbusha kuwa kazi hiyo ni ya kitaifa hivyo wanapaswa kutanguliza uzalendo, nidhamu na uwajibikaji ili kuhakikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 unamalizika kwa amani.
"Kura yako Haki yako Jitokeze kupiga Kura".
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe