Kitengo hiki kina jumla ya Watumishi Watatu (03), Wawili (02) wakiwa ni Wataalamu wa TEHAMA na Mmoja (01) akiwa ni Afisa Habari. Kitengo kinahusika na usimamiaji wa mifumo mbalimbali ya Halmashauri na kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya matumizi sahihi ya vifaa vya TEHAMA.
MAJUKUMU YA KITENGO CHA TEHAMA
Kutangaza shughuli zote za serikali na kuujulisha umma shughuli za maendeleo zinazotekelezwa katika Halmashauri kwa njia mbalimbali zikiwemo magazeti, majarida,vitabu, vipeperushi, radio, TV na Tovuti.
Majukumu mengine ya msingi ya Kitengo yanahusu kusimamia, kuratibu na ushauri wa matumizi ya teknolojia ya kompyuta. Kusimika Mfumo wa Kompyuta wa Kuhifadhi taarifa na Kumbukumbu za Watumishi na Mishahara (Intergrated Human Capital Management System); pamoja na utekelezaji wa Sera ya Serikali Mtandao (e-government policy) katika utumishi wa umma
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe