Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe, Bi. Kuruthum Sadick,Agosti 12,2025 ameagana na timu ya watumishi watakaoshiriki mashindano ya Shirikisho la Michezo Serikali za Mitaa (SHIMISEMITA) yatakayofanyika Jijini Tanga kuanzia Agosti 15 hadi 29, 2025.
Katika mashindano hayo yanayoongozwa na kaulimbiu isemayo “Jitokeze kupiga kura kwa maendeleo ya Michezo",Halmashauri ya Mji Njombe itashiriki kwenye mchezo wa mpira wa wavu(volleyball), mpira wa mikono (handball), pooltable na mchezo wa drafti.
Bi. Kuruthum amewataka washiriki wote kuonesha nidhamu, mshikamano na ushindani wa hali ya juu ili kuiwakilisha vema Halmashauri ya Mji Njombe.
Watumishi wa Serikali za Mitaa kutoka Halmashauri 184 za mikoa ya Tanzania watashiriki michezo mbalimbali katika mashindano hayo.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe