Katika kuadhimisha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama , Halmashauri ya Mji Njombe inaendelea kutoa elimu kwa wakina mama kuhusu umuhimu wa kunyonyesha maziwa ya mama ili kuimarisha afya ya mama na mtoto.
Afisa Lishe Bw. Michael Swai akitoa elimu ya umuhimu wa kunyonyesha maziwa ya mama kwa wakazi wa kijiji cha Lwangu kilichopo kata ya Kifanya Halmashauri ya Mji Njombe ,amesisitiza kuwa jamii ina wajibu wa kusaidia mama kwa kumpatia taarifa sahihi, msaada wa kihisia na kimazingira ili aweze kunyonyesha kwa mafanikio.
Maziwa ya mama ni kinga bora kwa mtoto dhidi ya magonjwa mengi na huimarisha uhusiano wa karibu kati ya mama na mtoto.
Kaulimbiu ya maadhimisho ya unyonyeshaji 2025 inasema ,"Thamini unyonyeshaji, weka mazingira wezeshi kwa mama na mtoto"
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe