Na,Mario Mgimba
Julai 4, 2025 Watendaji wa vijiji, mitaa na kata katika Halmashauri ya Mji Njombe wamepatiwa mafunzo maalumu juu ya utekelezaji na matumizi ya Mfumo wa Anwani za Makazi (NaPA).
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Mji Njombe, Samson Medda, aliwataka watendaji wote kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo kama ilivyokusudiwa huku akisisitiza utekelezaji wa mfumo huo ni agizo la serikali linalopaswa kuzingatiwa kwa umakini.
“Mfumo huu ni msingi wa maendeleo ya kidijitali na utaratibu wa kutoa huduma kwa wananchi ,Kwa mfano, wanafunzi waliomaliza kidato cha sita na wanaoomba mikopo ya elimu ya juu watapata msaada mkubwa kupitia mfumo huu kwa kurahisisha upitishaji wa taarifa zao,” alisema Medda Afisa Utumishi
Mafunzo hayo yamelenga kujenga uwezo wa kitaalamu kwa watendaji ili kuhakikisha kuwa mfumo huo unatekelezwa kwa ufanisi katika ngazi zote za utawala.
Aidha katika mfumo huo Watendaji wamefundishwa majukumu mbalimbali ya ikiwa ni pamoja na Utoaji na usajili wa majina ya barabara na mitaa ,Ukusanyaji na uhuishaji wa taarifa za Anwani za Makazi,
Uhamasishaji wa uwekaji wa vibao vya namba za nyumba na nguzo za majina ya barabara,kuweka mikakati ya ulinzi wa miundombinu ya mfumo huo, kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi ya Anwani za Makazi pamoja na Kuratibu utekelezaji wa mfumo katika maeneo yao ya kazi .
Mafunzo haya ni sehemu ya juhudi za kitaifa kuhakikisha kila mwananchi anapata anwani sahihi ya makazi, ambayo ni muhimu kwa mipango ya maendeleo, utoaji wa huduma bora na uboreshaji wa usalama.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe