• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu na uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mazingira na Usafishaji
      • Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu.
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Election
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Utamaduni,Sanaa na Michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

DC Njombe "Tujitokeze kuchanja, Chanjo ni Salama"

Tarehe iliyowekwa: October 6th, 2021

Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe. Kissa Gwakisa ameoneshwa kusikitishwa na mwamko mdogo wa Wananchi kujitokeza kuchanja katika Wilaya ya Njombe ambayo mpaka sasa Wilaya hiyo kushindwa kufanya vizuri kwenye zoezi la uchanjaji wa chanjo ya UVIKO 19 katika Mkoa wa Njombe na hivyo kufanya kikao hicho kwa lengo la kujengeana uwezo,kuhamasishana  na kufanya utekelezaji wa kuhakikisha chanjo zinafikia jamii na jamii inachanja.

Akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya CCM Wilaya, Waheshimiwa Madiwani na Wataalamu mbalimbali kutoka Halmashauri ya Mji Njombe Mkuu wa Wilaya ya Njombe amesema kuwa Wilaya ya Njombe bado ipo nyuma kwenye zoezi zima la uchanjaji jambo linaloishushia hadhi Wilaya hiyo kutokana na Wilaya hiyo kuwa inaongoza katika kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo na amewataka Viongozi na Wataalamu kuchukua hatua za haraka kwa kutoa elimu kwa jamii na kuhamasisha uchanjaji.

“Tunatamani tufike mahali maisha yarudie kama yalivyokuwa awali. Tuache kuvaa barakoa, kutumia vitakasa mikono na hii yote itafanikiwa kama tutachukua hatua za kuchanja.Tushirikiane kwa pamoja na tutoe elimu sahihi kwa jamii  juu ya chanjo ya UVIKO 19.”Alisema Mkuu wa Wilaya.

Awali akitoa taarifa ya hali ya uchanjaji katika Halmashauri ya Mji Njombe Mratibu Chanjo wa Halmashauri Simon Ngassa amesema kuwa malengo makuu ya chanjo ni kupambana na ugonjwa, kupunguza maambukizi ya Ugonjwa na kupunguza vifo vitokanavyo na UVIKO 19.

Naye Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya amesema kuwa changamoto kubwa zilizokuwepo katika zoezi hilo ilikuwa na uhamasishaji mdogo kwenye jamii,uwepo wa vituo vichache vya uchanjaji,ukosefu wa rasilimali na imani mbalimbali potofu kwa jamii juu ya chanjo.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Njombe Edward Mgaya amesema kuwa maendeleo ya Nchi yanatokana na watu na endapo watu watakufa kutokana na ugonjwa wa CORONA ilihali chanjo ipo hakutakuwepo na maendeleo kwenye Nchi.

“Kama tupo ndani ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi na tunatekeleza Ilani ya Chama hatuna budi kuelimisha jamii kuchukua hatua na kuchanja.Elimu ni jambo la pekee linalohitajika kwa jamii yetu ili waweze kuchanja.Naamini wengi wanapenda kuchanja ila ukosefu wa elimu ya kutosha ndio umepelekea zoezi hili kutokufanya vizuri katika Halmashauri yetu.”Alisema Mgaya.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmasahuri ya Mji Njombe Dkt. Yesaya Mwasubila  amesisitiza kuwa jamii imekuwa na iamani potofu na kuwa na hofu juu ya usalama wa chanjo hiyo ambapo amesema kuwa chanjo hiyo ni salama na imethibitishwa na Shirika la Afya duniani kuwa ni salama na mpaka sasa katika Halmashauri yake hajapokea malalamiko yoyote kwa watu waliochanjwa kudhurika au kupata matatizo yoyote yaliyosababishwa na chanjo hiyo.

Wakitoa michango yao kwa nyakati tofauti tofauti Diwani wa Kata ya Mjimwema Mahenge amesema kuwa kupitia kikao hicho nae amehamasika kwenda kuchanja na amesema kuwa ukosefu wa elimu sahii ndio kikwazo kikubwa kwenye zoezi zima la uchanjaji na kuomba elimu na huduma ya chanjo kuwafikia wananchi kwa karibu zaidi kupitia huduma tembezi.

Kwa upande wake Mheshimiwa Angela Mwangeni Viti Maalumu Njombe Mjini amesema kuwa yeye ni miongoni mwa watu waliohamasika na kupata chanjo na hii imetokana na elimu ambayo amekuwa akiipata ya umuhimu wa chanjo.

George Emmanuel Katibu Tawala Wilaya ya Njombe amewataka viongozi wa Halmashauri ya Mji Njombe wakiwemo Waheshimiwa Madiwani kuhakikisha kuwa  wanaonyesha njia kwa jamii kwani jamii imekuwa ikiwatazama viongozi hao kwa yale wanayoyafanya na kuwataka kueneza mazuri ya chanjo kwa jamii na kuihamasisha jamii kuchanja na kutoa elimu potofu zilizojengeka miongoni mwa Wananchi.

Mpaka sasa Halmashauri ya Mji Njombe inavituo 71 vya kutolea chanjo vituo 45 vikiwa vinatoa huduma ya chanjo kila siku ambapo mpaka kufikia tarehe 04/10/2021 idadi ya watu waliochanja ni 1621 ambayo ni sawa na asilimia 35.1 ya lengo ya dozi iliyotolewa ambapo mikakati iliyofikiwa katika kikao hicho ni kuendelea kutoa elimu na kusambaza chanjo kwa Kata zote 13 ili kurahisisha upatikanaji.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI. June 17, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UBORESHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA. December 20, 2024
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. April 18, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • SALAMU ZA SHUKRANI

    July 01, 2025
  • SIKU NNE ZA KUSIKILIZA KERO NA MAONI YA WANANCHI LIMEHITIMISHWA KWA MAFANIKIO.

    June 30, 2025
  • Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe atoa wito kwa Wananchi kujitokeza kupata huduma Stendi ya Zamani.

    June 27, 2025
  • HALMASHAURI YA MJI NJOMBE YAPONGEZWA KWA HATI SAFI

    June 17, 2025
  • Angalia zote

Video

LUNYANYWI FISH FARM YASHUGHULIKIA KERO ZA WAFUGAJI WA SAMAKI NJOMBE TC
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe