Zoezi la kusikiliza kero na kupokea maoni ya wananchi wa Halmashauri ya Mji Njombe, lililoanza rasmi tarehe 27 Juni 2025, limehitimishwa tarehe 30 Juni 2025 kwa mwitikio mkubwa
Zoezi hilo limefanyika katika eneo la stendi ya zamani, Njombe Mjini, na limekuwa na mafanikio makubwa huku wananchi wengi wakijitokeza kwa wingi kutumia fursa hiyo kuwasilisha matatizo na changamoto mbalimbali zinazowakabili katika maeneo yao.
Timu ya wataalamu wa Halmashauri ya Mji Njombe imepokea maoni moja kwa moja kutoka kwa wananchi na kutoa majibu ya papo kwa papo kwa baadhi ya changamoto, huku nyingine zikichukuliwa kwa hatua zaidi za kiserikali.
Wananchi wamepongeza juhudi hizi na kueleza kuwa ni hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano kati ya serikali na wananchi, pamoja na kuhakikisha huduma za kijamii zinaboreshwa kwa mujibu wa mahitaji ya jamii.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe