Juni 27, 2025 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Bi. Kuruthum Sadick amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kupata huduma mbalimbali zinazotolewa katika mabanda maalumu yaliyoandaliwa katika eneo la stendi ya zamani mjini Njombe.
Akizungumza Juni 27,2025 Juni wakati wa ukaguzi wa mabanda hayo, Mkurugenzi amesema lengo la utoaji wa huduma hizo ni kuwasogezea wananchi huduma muhimu karibu na maeneo yao ya makazi na biashara, na kuhakikisha kila mwananchi anapata haki na huduma stahiki.
"Ni fursa kwa kila mwananchi kufika stendi ya zamani ,Tumeamua kuwafuata wananchi kutoa eliu mbalimbali na Kupokea ushauri ,kusikiliza changamoto zao, kutoa elimu, kwa ukaribu zaidi," alisema Mkurugenzi Halmashari ya Mji Njombe
Huduma zinazotolewa katika mabanda hayo ni pamoja na huduma za afya, ardhi, biashara, usafi wa mazingira, mapato, sheria, malalamiko ya wananchi, usuluhishi wa migogoro, masuala ya utumishi pamoja na huduma kwa wateja.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe