• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu na uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mazingira na Usafishaji
      • Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu.
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Election
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Utamaduni,Sanaa na Michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

TASAF kuvinoa vikundi vya Wanufaika kuhusu kuweka akiba na kukuza uchumi

Tarehe iliyowekwa: June 17th, 2019

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Nchini TASAF umeendelea kuwawezesha wanufaika wa  mpango wa kunusuru kaya maskini kupitia mpango wa kuweka akiba na kukuza uchumi lengo ikiwa ni kuhamasisha walengwa kuunda vikundi na kuimarisha uchumi wa kaya zao.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya kuwajengea uwezo wawezeshaji ngazi ya Halmashauri kuhusu uhamasishaji wa uundwaji wa vikundi vya kuweka akiba na kukuza uchumi, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Ndg. Thadei Luoga amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu na ni vyema washiriki wakaelewa na kwenda kuwafundisha wanufaika ipasavyo ili waweze kuondokana na wimbi la umaskini.

“Wapo ambao wamekuwa wakibeza kuwa programu hii haichangii chochote. Hii sio kweli. Wananchi  wamekuwa wakifanya shughuli mbalimbali za maendeleo lakini wakati mwingine kwa kukosa uelewa wa namna ya kuweka akiba na kutunza kumbukumbu zao wamekuwa wakiishia kwenye wimbi la umaskini wa kipato au lishe. TASAF wanatujengea uwezo ili tuweze kuwapelekea wanufaika na waweze kufanyia kazi.”Alisema Luoga

Thomas Mwakagali ambaye ni Mwezeshaji ngazi ya Halmashauri kutoka Kata ya Makowo amesema kuwa TASAF imekuwa ikitoa mafunzo hayo mara kwa mara lengo ikiwa ni kuwakumbusha wanufaika wa mpango wa TASAF kutengeneza vikundi ambavyo kupitia fedha za ruzuku wanazopokea kuweza kuweka akiba kwa ajili ya kujiimarisha kiuchumi.

“Tumekuwa tukitoa elimu hii kwa wanufaika. Kupitia fedha za ruzuku tumekuwa tukiwahamasisha juu ya uundwaji wa vikundi vya kuweka akiba na kukuza uchumi. Kupitia fedha ambazo wamekuwa wakipokea kila baada ya miezi miwili ambapo wapo walengwa wanaopokea kiasi cha Shilingi elfu ishirini, wengine thelathini ni kiasi kidogo lakini elimu hii imewajenge nidhamu ya kutunza na kuweka akiba ambapo mpaka sasa tunavikundi vyenye milioni tano, milioni mbili. Haya yote ni manufaa ya elimu hii ya akiba.”Alisema Mwakagali.

Halmashauri ya Mji Njombe ina jumla ya wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini 3381 ambapo jumla ya vikundi 123 vya akiba vimeshaundwa na kupatiwa masanduku ya kuhifadhia hela na shajara mbalimbali.

 

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI. June 17, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UBORESHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA. December 20, 2024
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. April 18, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • ASILIMIA 100 WAFAULU KIDATO CHA SITA – MIUNDOMBINU WEZESHI NA MOTISHA YATAJWA KUWA CHACHU YA MAFANIKIO

    July 09, 2025
  • WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA ANWANI ZA MAKAZI.

    July 05, 2025
  • RUZUKU YA CHANJO YA MIFUGO,KINGA KWA MAENDELEO YA MIFUGO

    July 05, 2025
  • Dkt. Mhede azindua zoezi la chanjo ya ruzuku kwa mifugo Halmashauri ya Mji Njombe, dozi 227,000 kutolewa kwa ng'ombe na kuku

    July 05, 2025
  • Angalia zote

Video

ZIFAHAMU FAIDA ZA HERENI YA KIELEKTRONIKI KWA NG'OMBE.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe