Afisa Nyuki kutoka Halmashauri ya Mji Njombe Bi.Mary Urasa ,akiendelea kutoa elimu ya ufugaji nyuki kibiashara kwa wananchi na wadau mbalimbali wanaotembelea banda la Halmashauri katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Wananchi wamepatiwa uelewa kuhusu:
• Mbinu bora za ufugaji wa nyuki ili kuongeza uzalishaji wa asali na mazao mengine ya nyuki.
• Umuhimu wa ufugaji nyuki katika kulinda mazingira na kuongeza kipato cha kaya.
• Fursa za masoko ya bidhaa za nyuki ndani na nje ya nchi.
• Uchakataji na uhifadhi wa mazao ya nyuki.
Wananchi wote mnakaribishwa kuendelea kutembelea banda la Halmashauri ya Mji Njombe ili kupata elimu hii na nyingine kwenye kilimo,mifugo na uvuvi kwa maendeleo endelevu.
"Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025".
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe