Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Jabir Makame ametembelea banda la maonesho ya Nanenane la Halmashauri ya Mji Njombe, na kujionea fursa mbalimbali za maendeleo na ubunifu wa kilimo zinazotolewa na wakulima na wafugaji wa halmashauri hiyo.
Akizungumza , Mhe. Makame alipotembela banda hilo alisisitiza umuhimu wa kutumia teknolojia na maarifa ya kisasa katika kuongeza tija kwenye kilimo na ufugaji.
"Nipongeze Halmashauri ya Mji Njombe imeonyesha mfano bora wa jinsi gani wakulima , wafugaji na wajasirasilimali wanatumika katika kuboresha maisha ya wananchi ,hivyo wataalamu Tunapaswa kuendeleza jitihada hizi kwa kuwashirikisha katika sekta ya kilimo." Alisema Makame Mkuu wa Mkoa Swongwe.
Maonesho ya Nanenane mwaka 2025 yamejikita kwenye kaulimbiu ya: "Chagua viongozi bora kwa maendeleo endelevu ya kilimo ,mifugo na uvuvi 2025"
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe