Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Beno Malisa, Agosti 2,2025 amefungua rasmi Maonesho ya 88 ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya. Ufunguzi huo umefanyika kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa aliyetarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Miongoni mwa maagizo yaliyotolewa wakati wa ufunguzi huo ni pamoja na ;
• Usimamizi wa matumizi bora ya ardhi ili kuzuia migogoro.
• Kuzingatia usalama wa chakula.
• Matumizi sahihi ya viuatilifu na kemikali katika shughuli za kilimo na ufugaji,
• Halmashauri kuanzisha benki ya ardhi ili kuwezesha vijana kuwekeza.
• Kusimamia wakulima kutoanza kuvuna mazao kabla ya wakati.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi kutoka mikoa mbalimbali ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, washiriki wa maonesho, waoneshaji pamoja na wananchi.
Kauli mbiu ya maonesho ya nanenane mwaka huu ni,"Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025."
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe