Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Bi.Kuruthum Sadick ametembelea banda la Halmashauri kwenye Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale, Jijini Mbeya.
Mkurugenzi amejionea namna wakulima na wafugaji wanavyotekeleza shughuli zao kwa ubunifu na tija, pamoja na faida wanazozipata kupitia sekta ya kilimo,mifugo uvuvi na ujasiriamali. Amesisitiza dhamira ya Halmashauri kuendelea kuwawezesha wakulima na wajasiriamali kwa elimu, mbinu bora ,mikopo na fursa za masoko ili kuongeza uzalishaji na kipato.
Aidha, amewakaribisha wananchi wote wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kutembelea banda la Halmashauri ya Mji Njombe ili kujifunza, kuhamasika na kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na wataalamu waliopo.
Halmashauri ya Mji Njombe inajivunia kutoa wakulima na wafugaji hodari wanaoshiriki mashindano kikanda wakiwemo:
• Julius Mlelwa mfugaji wa Ng’ombe wa nyama kutoka kata ya Kifanya.
• Aloisia Mdenye mfugaji wa Ng’ombe wa maziwa ,kutoka kata ya Yakobi.
• Nuru kihombo mfugaji wa kuku wa mayai ,kutoka kata ya Mjimwema.
• Modestus Ng'ande mkulima wa mahindi kutoka kata ya Ramadhani na,
• Steven Mlimbila mkulima wa parachichi kutoka Kata ya Ramadhani.
Maonesho yanaendelea na yanatarajiwa kufikia kilele tarehe 8 Agosti 2025,yakiongozwa na kaulimbiu inayosema;"Chagua viongozi Bora kwa Maendeleo endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025".
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe