Kuelekea awamu ya pili ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura na kuweka wazi daftari la awali,leo
Aprili 24,2025 Afisa mwandikishaji Jimbo la Njombe Mjini Ndg.Samson Medda, amekutana na viongozi wa vyama vya siasa katika kikao kilicholenga kuwapa taarifa muhimu kuhusu awamu ya pili ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Medda alitumia fursa hiyo kuwahimiza viongozi hao kuandaa mawakala ambao watashiriki kusimamia zoezi hilo katika vituo kwa kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).Aidha kuwahamasisha wananchi wote wanaoguswa na zoezi hilo kujitokeza ili waweze kupata fursa yakushiriki Uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.
Vyama vya siasa ni wadau muhimu katika mchakato mzima wa uchaguzi unaohusisha uandikishaji wa wapiga kura wapya pamoja na uboreshaji wa taarifa za awali katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Awamu ya pili ya uboreshaji Jimbo la Njombe Mjini itafanyika kwa siku saba kuanzia Mei 1 - 7,2025 kwenye vituo vilivyoanishwa kwenye kata zote 13 za Halmashauri ya Mji Njombe.
"Kujiandikisha kuwa mpiga kura ni msingi wa Uchaguzi bora".
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe