• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu na uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mazingira na Usafishaji
      • Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu.
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Election
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Utamaduni,Sanaa na Michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

Agizo la Rais Magufuli Njombe latekelezwa,Stendi Kuu Mpya yaanza kazi rasmi leo.

Tarehe iliyowekwa: May 11th, 2019

Kufuatia agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli la kutaka stendi kuu mpya  ya Njombe  kuanza kutumika ifakapo May 11,2019 hatimae stendi hiyo imeanza kazi rasmi leo.

Akizingumza na Waandishi wa Habari, Abiria  na Wananchi  waliofika katika stendi hiyo  mpya, Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Ruth Msafiri amewapongeza Wananchi kwa kuitikia wito wa kuhamia katika stendi mpya licha ya kuwepo na shughuli za umalizia wa ujenzi wa stendi hiyo zikiendelea.

“Nawapongeza Wananchi kwa kujitokeza kwa wingi. Wengi mmekuja kushuhudia kama kweli stendi imeanza lakini pia kwa wasafiri, wadau wa vyombo vya usafirishaji mwitikio umekuwa mkubwa na hii inaonesha wazi jinsi mlivyokuwa na kiu ya siku nyingi kuitumia stendi hii” Alisema MKuu wa Wilaya.

Mkuu wa Wilaya aliongezea kuwa”Tunamshukuru Mhe. Rais kwani kupitia maelekezo yake  kumefanya stendi hii ianze kufanya kazi. Ametusaidi sana katika kutusukuma katika siku hizi za mwishoni  na leo tumetekelza agizo lake stendi imeanza kufanya kazi na Wananchi wanafuraha iliyopitiliza” Alisema

Johanes Kyelula ni Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na Usalama wa Stendi ambaye yeye  alisema kuwa anaipongeza  Halmashauri kwa kufanikiwa kuanza kutumika kwa  stendi hiyo kama alivyo agiza Rais na watahakikisha kuwa wanasimamia ulinzi ndani ya stendi na kuhakikisha kuwa nidhamu katika stendi mpya inakuwepo ikiwa ni sambamba na kuwachukulia hatua na wote watakaotoa lugha za matusi kwa abiria au kuona watu wasio na nia njema ya  kuwaibia abiria kwenye stendi hiyo.

Glory Sanga ni mmojawapo wa wafanyakazi katika mabasi yanayofanya safari zake nje ya Mkoa wa Njombe  ambaye yeye amesema kuwa stendi mpya mpaka kukamilika kwake itakuwa ni miongoni mwa stendi bora na zenye viwango vya  hali ya juu ukilinganisha na Mikoa ambayo amekuwa akipita yenye stendi.

“Mimi ni Kondakta na nimekuwa nikisafiri Mikoani nimeona utofauti wa stendi hii na hizo za Mikoa mingine. Stendi hii imejengwa kwenye ubora hata ukiangalia kwa macho. Japokuwa haijakamilika yote, ni matumaini yangu itakapo kamilika yote itakuwa ni miongoni mwa stendi za kuigwa katika Tanzania. Naipongeza Halmashauri ambao ndio wasimamizi wa ujenzi wa stendi kwa kazi nzuri” Alisema Glory

John Msemwa miongoni mwa abiria walifika kwenye stendi mpya leo amesema kuwa changamoto nyingi kwa sasa zimepungua ukilinganisha na stendi ya awali.

“Kwanza stendi ya zamani ilikuwa ndogo sana hii stendi ni kubwa, miundombinu ni mizuri vyoo maji yapo vyoo vizuri, visafi hata ukiangalia huku hakuna matope kama kule kwenye stendi ya mwanzo. Stendi ya awali matope mengi hasa wakati wa mvua hakuna hata sehemu ya kukaa. Huku kuna maeneo mengi ya kukaa ikikamilika itakuwa kivutio cha watalii wa ndani” Alisema Msemwa.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Illuminatha Mwenda alisema kuwa mpaka sasa ujenzi wa stendi hiyo umekamilika kwa asilimia 95 na amesema kuwa shughuli zolizosalia zinatarajia kukamilishwa ndani ya wiki mbili zijazo.

“Tunashukuru kwa pongezi kwani haikuwa kazi rahisi. Asilimia tano zilizosalia tutazikamilisha ndani ya wiki mbili. Licha ya mabasi kuanza tulikuwa pia na kikao na wahandisi ili kuona ni namna gani kazi zilizosalia tunazikamilisha ndani ya wiki mbili licha ya kuwepo na changamoto ya mvua za mara kwa mara.”Alisema Mwenda

Mwenda aliongezea kuwa licha ya kutoa huduma kwa wWananchi stendi hiyo pia ni chanzo kikuu cha mapato kwa Halmashauri na wanataraji kukusanya milioni mia tatu kwa mwaka hayo yakiwa ni makisio ya chini.

Mkurugenzi huyo pia aliendelea kuwasisitizia wananchi kuhakikisha kuwa wanafuata utaratibu uliowekwa wa kuchangia gharama ya Tsh 200 kwa wale ambao wanaingia stendi pasipokuwa na tiketi ya abiria.

Akiongelea suala wa Wajasiriamali wadogo  Bi Mwenda alisema umeandaliwa utaratibu mzuri na punde wataelekezwa utaratibu kwa wajasiriamali hao na amewasisitiza kuhakikisha kuwa wanakuwa na kitambulisho cha wajasiriamali.Mwenda amewapongeza wananchi kwa mwitikio wao na kusema kuwa ataendelea kutoa tarifa ya mabadiliko yoyote yatakayokuwepo katika stendi hiyo kadri muda unavyozidi kwenda na kwa kadri ya matengenezo yanayoendelea katika stendi hiyo.

Ikumbukwe kuwa Halmashauri ya Mji Njombe ni miongoni mwa Halmashauri 18 Nchi zinazonufaika na mradi wa uboreshaji  na uimarishaji Miji ambapo kwa upande wa Halmashauri ya Mji Njombe inatekeleza ujenzi wa soko la kisasa na ujenzi wa stendi kuu ya mabasi ambapo kwa upande wa stendi inakadiriwa kutumia bilioni 9 mpaka kukamilika kwake.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI,UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI. April 25, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UBORESHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA. December 20, 2024
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. April 18, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKUU WA WILAYA NJOMBE MHE. JUMA SWEDA ATOA WITO KUHUSU CHANJO YA PILI YA POLIO.

    April 29, 2025
  • AFISA MWANDIKISHAJI JIMBO LA NJOMBE MJINI AKUTANA NA VYAMA VYA SIASA

    April 24, 2025
  • ZIARA YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YA NJOMBE KUKAGUA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2025

    April 04, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Njombe awaonya wenyeviti kuhusu uharibifu wa miradi ya maendeleo

    February 15, 2025
  • Angalia zote

Video

WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA KUJITUMA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe