Watumishi ajira mpya Halmasahuri ya Mji Njombe Januari 25,2024 wamepewa mafunzo maalumu yakuwatambulisha kwenye utumishi wa Umma .
Mafunzo hayo yanalenga kuwapatia uelewa wa sheria ,kanuni,na taratibu mbalimbali za utumishi wa umma ili waweze kufahamu haki zao katika utumishi wa umma.
Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe ,Samson Medda Mkuu wa Idara ya Utumishi na Rasilimali Watu Halmashauri ya Mji Njombe ,amewataka watumishi hao wa ajira mpya kuzingatia mafunzo watakayopatiwa na kuwa waadilimu kwenye utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku kwa mujibu misingi,kanuni taratibu na sheria za utumishi wa umma.
Mafunzo hayo ya siku mbili yanayotolewa na maafisa utumishi mbalimbali wa Halmashauri ya Mji Njombe yatahitimishwa kwa watumishi hao kuapa kiapo cha uadilifu Januari 26,2024.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe