Februari 25,2024 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Ndugu Kuruthum Sadick, amezindua awamu ya tatu ya zoezi la ugawaji wa kinga tiba dhidi ya Usubi kwa Halmashauri ya Mji Njombe.
Uzinduzi huo umefanyika katika kanisa la Tanzania Assembles of God (TAG) lililopo Melinze.
Bi. Kuruthum ametoa rai kwa wananchi kuhakikisha wanameza kinga tiba hiyo ambayo ni salama kwa afya na inatolewa bure.
Jumla ya watu 160 wamepatiwa kinga tiba siku ya ufunguzi na zoezi hili linaendelea hadi Machi 02, 2024 kwa wagawa dawa kupitia nyumba kwa nyumba ambapo walengwa ni wenye umri kuanzia miaka 5 isipokuwa wajawazito na wagonjwa mahututi.
Usubi ni ugonjwa unaosababishwa na minyoo huenezwa na inzi weusi wanaoishi kandokando ya mito yenye maji Safi yaendayo kasi. Athari za ungonjwa wa usubi ni pamoja na kupata ulemavu wa kudumu.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe